Misaada ya Kujifunza
Marsh, Thomas B.


Marsh, Thomas B.

Rais wa Kwanza wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili baada ya Urejesho wa Kanisa katika mwaka 1830. Alishikilia funguo za ufalme kwa niaba ya wale Kumi na Wawili (M&M 112:16) na, katika mwaka 1838, aliamriwa kwa ufunuo kuchapisha neno la Bwana (M&M 118:2). Sehemu ya 31 ya Mafundisho na Maagano inaelekezwa kwake yeye. Marsh alitengwa na Kanisa katika mwaka 1839 lakini alibatizwa upya tena katika mwezi wa Julai 1857.