Misaada ya Kujifunza
Har-Magedoni


Har-Magedoni

Jina Har-Magedoni linatoka katika neno la Kiebrania Har-Megidoni maana yake “mlima wa Megido.” Bonde la Megido lipo katika sehemu ya magharibi mwa mbuga za Esdraloni, maili hamsini (kilometa themanini) kaskazini ya Yerusalemu, na ni sehemu ya mapigano kadhaa muhimu katika nyakati za Agano la Kale. Pigano kuu na la mwisho ambalo litakuwepo karibu na wakati wa Ujio wa Pili wa Bwana linaitwa vita vya Har-Magedoni kwa sababu vitaanzia mahali hapa. (Ona Eze. 39:11; Zek. 12–14, hususani 12:11; Ufu. 16:14–21.)