Misaada ya Kujifunza
Ukuhani wa Haruni


Ukuhani wa Haruni

Ukuhani mdogo (Ebr. 7:11–12; M&M 107:13–14). Ofisi zake ni askofu, kuhani, mwalimu, na shemasi (M&M 84:30; 107:10, 14–15, 87–88). Hapo zamani, chini ya sheria za Musa, palikuwepo na makuhani wakuu, makuhani, na Walawi. Kwa sababu Waisraeli wa kale walimwasi Mungu. Musa nan a ukuhani mtakatifu waliondolewa kutoka kwao na ukuhani mdogo uliendelea. Wao walikataa kutakaswa na kupokea Ukuhani wa Melkizedeki na ibada zake. (Ona M&M 84:23–26.) Ukuhani wa Haruni hushughulikia ibada za kimwili na za nje katika sheria ya injili (1 Nya. 23:27–32; M&M 84:26–27; 107:20). Una shikilia funguo za huduma ya malaika, za injili ya toba, na ubatizo (M&M 13). Ukuhani wa Haruni ulirejeshwa duniani katika kipindi hiki 15 Mei 1829, Yohana Mbatizaji aliwatunukia Joseph Smith na Oliver Cowdery jirani na Harmony, Pennsylvania (M&M 13; JS—H 1:68–73).