Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 13


Sehemu ya 13

Dondoo kutoka katika historia ya Joseph Smith inayoeleza kutawazwa kwa Nabii na Oliver Cowdery kwenye Ukuhani wa Haruni jirani na Harmony, Pennsylvania, 15 Mei 1829. Kutawazwa huko kulifanywa kwa mikono ya malaika ambaye alijitambulisha kama Yohana, yule yule ambaye anaitwa Yohana Mbatizaji katika Agano Jipya. Malaika alieleza kwamba yeye alikuwa akiyafanya chini ya maelekezo ya Petro, Yakobo na Yohana, Mitume wa kale walioshikilia funguo za ukuhani wa juu zaidi, ambao uliitwa Ukuhani wa Melkizedeki. Ahadi ilitolewa kwa Joseph na Oliver kwamba katika wakati upasao ukuhani huu mkuu utatunukiwa kwao. (Ona sehemu ya 27:7–8, 12.)

Funguo na uwezo wa Ukuhani wa Haruni zinatolewa.

1 Juu yenu ninyi watumishi wenzangu, katika jina la Masiya aninawatunukia bUkuhani wa Haruni, ambao hushikilia funguo za huduma za cmalaika, na za injili ya dtoba, na za eubatizo kwa uzamisho kwa ajili ya ondoleo la dhambi; na hizi kamwe hazitaondolewa tena kutoka duniani, mpaka fwana wa Lawi watakapotoa tena matoleo kwa Bwana katika ghaki.