Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 107


Sehemu ya 107

Ufunuo juu ya ukuhani, uliotolewa kupitia Joseph Smith Nabii, huko Kirtland, Ohio, mnamo Aprili 1835. Ingawa sehemu hii iliandikwa mwaka 1835, kumbu kumbu za kihistoria zinasisitiza kwamba sehemu kubwa za aya ya 60 hadi 100 zinajumuisha ufunuo uliotolewa kupitia kwa Joseph Smith 11 Novemba 1831. Sehemu hii ilihusiana na kuanzishwa kwa Akidi ya Kumi na Wawili katika Februari na Machi 1835. Yaelekea Nabii aliisoma mbele ya wale waliokuwa wakijitayarisha kuondoka 3 Mei 1835, katika misheni yao ya kwanza kama akidi.

1–6, Kuna ukuhani wa aina mbili: wa Melkizedeki na wa Haruni; 7–12, Wale walio na ukuhani wa Melkizedeki wanao uwezo wa kufanya kazi katika ofisi zote katika Kanisa; 13–17, Uaskofu husimamia Ukuhani wa Haruni, ambao huhudumu katika ibada za kimwili; 18–20, Ukuhani wa Melkizedeki hushikilia funguo za baraka zote za kiroho; Ukuhani wa Haruni unashikilia funguo za kuhudumiwa na malaika; 21–38, Urais wa Kwanza, Mitume Kumi na Wawili, na Sabini huunda akidi za kuongoza, ambazo maamuzi yake yatafanywa katika umoja na haki; 39–52, Utaratibu wa kipatriaki unaelezwa kutoka Adamu hadi Nuhu; 53–57, Watakatifu wa zamani walikusanyika huko Adamu-ondi-Ahmani, na Bwana akawatokea; 58–67, Mitume Kumi na Wawili watawaweka maofisa wa Kanisa katika mpangilio unaostahili; 68–76, Maaskofu hutumika kama waamuzi wa wote katika Israeli; 77–84, Urais wa Kwanza na Mitume Kumi na Wawili huunda mahakama ya juu katika Kanisa; 85–100, Marais wa Ukuhani hutawala akidi zao husika.

1 Katika kanisa, zipo aina mbili za Ukuhani, nazo, ni aMelkizedeki na bHaruni, ukijumuisha na Ukuhani wa Lawi.

2 Kwa nini wa kwanza unaitwa Ukuhani wa aMelkizedeki ni kwa sababu Melkizedeki alikuwa kuhani mkubwa sana.

3 Kabla ya siku zake ulikuwa ukiitwa Ukuhani Mtakatifu, kwa aMfano wa Mwana wa Mungu.

4 Lakini kwa sababu ya heshima au aunyenyekevu kwa jina la Kiumbe Mkuu, ili kuepuka kurudiwa mara kwa mara kwa jina lake, wao, kanisa, katika siku za kale, waliuita ukuhani huo Melkizedeki, au Ukuhani wa Melkizedeki.

5 Mamlaka nyingine zote au ofisi zote katika kanisa ni aviambatanisho kwenye ukuhani huu.

6 Lakini ziko sehemu kuu au vichwa vikuu viwili—cha kwanza ni ukuhani wa Melkizedeki, na kingine ni Ukuhani wa Haruni au aUkuhani wa Lawi.

7 Ofisi ya amzee huja chini ya ukuhani wa Melkizedeki.

8 Ukuhani wa Melkizedeki unashikilia haki ya Urais, na unao uwezo na amamlaka juu ya ofisi zote katika kanisa katika vipindi vyote vya ulimwengu, kuhudumu katika mambo ya kiroho.

9 aUrais wa Ukuhani Mkuu, kwa mfano wa Melkizedeki, unayo haki ya kutenda kazi katika ofisi zote katika kanisa.

10 aMakuhani wakuu kwa mfano wa Ukuhani wa Melkizedeki wanayo bhaki ya kutenda kazi katika nafasi yao wenyewe, chini ya maelekezo ya urais, katika kuhudumu katika mambo ya kiroho, na pia katika ofisi ya mzee, kuhani (wa mfano wa Lawi), mwalimu, shemasi, na muumini.

11 Mzee anayo haki ya kutenda kazi kwa niaba yake wakati kuhani mkuu hayupo.

12 Kuhani mkuu na mzee watahudumu katika mambo ya kiroho, kulingana na maagano na amri za kanisa; na wanayo haki ya kutenda kazi katika ofisi hizi zote za kanisa iwapo hakuna wenye mamlaka ya juu zaidi.

13 Ukuhani wa pili unaitwa aUkuhani wa Haruni, kwa sababu ulitolewa kwa bHaruni na uzao wake, katika vizazi vyao vyote.

14 Kwa nini unaitwa ukuhani mdogo ni kwa sababu ni akiambatanisho kwa ule mkubwa, au Ukuhani wa Melkizedeki, na unao uwezo wa kuhudumu katika ibada za nje.

15 aUaskofu ni urais wa ukuhani huu, na unashikilia funguo, au mamlaka hayo.

16 Hakuna mtu aliye na haki kisheria kwenye ofisi hii, kushikilia funguo za ukuhani huu, isipokuwa ni amzaliwa halisi wa ukoo wa Haruni.

17 Lakini kama kuhani mkuu wa Ukuhani wa Melkizedeki anayo mamlaka ya kutenda kazi katika ofisi ndogo zote, anaweza kutenda kazi katika ofisi ya askofu ikiwa hakuna mzaliwa halisi wa ukoo wa Haruni anayeweza kupatikana, ili mradi awe ameitwa na kuwekwa rasmi na akutawazwa katika uwezo huu kwa mikono ya bUrais wa Ukuhani wa Melkizedeki.

18 Uwezo na mamlaka ya ule wa juu, au Ukuhani wa Melkizedeki, ni kushikilia afunguo za baraka zote za kiroho za kanisa—

19 Kuwa na haki ya kupokea asiri za ufalme wa mbinguni, mbingu kufunuliwa kwao, kuwasiliana na baraza bkuu na kanisa la Mzaliwa wa Kwanza, na kufurahia ushirikiano wao na uwepo wa Mungu Baba, na Yesu aliye cmpatanishi wa agano jipya.

20 Uwezo na mamlaka ya ule mdogo, au Ukuhani wa Haruni, ni kushikilia afunguo za huduma ya malaika, na kufanya huduma ya bibada za kimwili, andiko la injili, cubatizo wa toba kwa dondoleo la dhambi, sawa sawa na maagano na amri.

21 Kuna umuhimu wa kuwepo kwa marais, au maofisa viongozi kutoka, au kuteuliwa au kutoka miongoni mwa wale ambao wametawazwa kwenye ofisi mbali mbali katika aina hizi mbili za ukuhani.

22 Wa aUkuhani wa Melkizedeki, bMakuhani Wakuu Viongozi watatu, waliochaguliwa na kikundi, kuteuliwa na kutawazwa katika ofisi hiyo, na ckuungwa mkono wa kuaminiwa, imani, na sala ya kanisa, hufanya akidi ya Urais wa Kanisa.

23 Wajumbe akumi na wawili wasafirio huitwa kuwa bMitume Kumi na Wawili, au mashahidi maalumu wa jina la Kristo ulimwenguni kote—hivyo kuwa tofauti na maofisa wengine katika kanisa katika majukumu ya wito wao.

24 Nao hufanya akidi, sawa sawa katika mamlaka na uwezo na marais wale watatu waliotajwa awali.

25 aSabini pia huitwa kuihubiri injili, na kuwa mashahidi maalumu kwa Wayunani na ulimwenguni kote—hivyo kuwa tofauti na maofisa wengine katika kanisa katika majukumu ya wito wao.

26 Nao wanafanya akidi, sawa sawa katika mamlaka na ile ya mashahidi maalumu Kumi na Wawili au Mitume ambao tumewataja sasa hivi.

27 Na kila uamuzi unaofanywa na akidi yoyote kati ya hizi lazima uwe kwa kura ya wengi wao, maana yake, kila mshiriki katika kila akidi, lazima akubaliane na maamuzi yake, ili kufanya maamuzi yao yawe na uwezo sawa au yawe na uhalali, yakubalike kwa kila mmoja—

28 Wengi wanaweza kuunda akidi ikiwa hali inafanya kutowezekana kuwa vinginevyo—

29 Kama si hivyo, maamuzi yao hayastahili baraka hizo ambazo maamuzi ya akidi ya marais watatu waliyatoa hapo awali, ambao walitawazwa kwa mfano wa Melkizedeki, na walikuwa watu wema na watakatifu.

30 Maamuzi ya akidi hizi, au mojawapo, yanapaswa kufanywa katika ahaki tupu, katika utakatifu, na kwa unyenyekevu wa moyo, kwa upole, na kwa uvumilivu, na katika imani, na bwema, na maarifa, kiasi, saburi, uchamungu, upendo wa kidugu na hisani;

31 Kwa sababu ahadi ni, kama mambo haya yamejaa tele kwao hawatakuwa watu wasio na amatunda katika maarifa ya Bwana.

32 Na ikiwa uamuzi wowote wa akidi hizi umefanywa pasipo haki, unaweza kuletwa mbele ya mkutano mkuu wa akidi hizi kadhaa, ambazo zinaundwa na wenye mamlaka za kiroho za kanisa; vinginevyo hapawezi kuwa na rufaa yoyote kutoka kwenye uamuzi wao.

33 Hawa Kumi na Wawili ndiyo Baraza Kuu la Viongozi Wasafirio, ili kutenda kazi katika jina la Bwana, chini ya maelekezo ya Urais wa Kanisa, kulingana na sheria za mbinguni; ili kulijenga kanisa, na kurekebisha masuala yote yalihusuyo katika mataifa yote, kwanza kwa aWayunani na pili kwa Wayahudi.

34 Sabini watatenda kazi katika jina la Bwana, chini ya maelekezo ya aKumi na Wawili au baraza kuu lenye kusafiri, katika kulijenga kanisa na kurekebisha mambo yote yalihusuyo katika mataifa yote, kwanza kwa Wayunani na halafu kwa Wayahudi—

35 Kumi na Wawili wakiwa wametumwa nje, wakiwa na funguo, kufungua mlango kwa utangazaji wa injili ya Yesu Kristo, na kwanza kwa Wayunani na halafu kwa Wayahudi.

36 aBaraza kuu la kudumu, katika vigingi vya Sayuni, huunda akidi iliyo sawa katika mamlaka katika mambo ya kanisa, katika maamuzi yao yote, na akidi ya urais, au baraza kuu lisafirilo.

37 Baraza kuu katika Sayuni huunda akidi yenye mamlaka sawa katika mambo ya kanisa, katika maamuzi yao yote, na mabaraza ya Kumi na Wawili katika vigingi vya Sayuni.

38 Ni kazi ya baraza kuu lenye kusafiri kuwaita hawa aSabini, wakati wanapohitaji msaada wa kujaza nafasi za miito mbalimbali kwa ajili ya kuhubiri na kusimamia injili, badala ya mwingine yeyote.

39 Ni wajibu wa Kumi na Wawili, katika matawi makubwa yote ya kanisa, kuwatawaza wahudumu awainjilisti, kulingana na wao watakavyo julishwa kwa ufunuo—

40 Mfano wa ukuhani huu ulithibitishwa kutolewa kutoka baba kwenda kwa mwana, na kisheria ni mali ya wazao halisi wa uzao mteule, ambao kwao ahadi zilifanywa.

41 Mfano huu ulianzishwa katika siku za aAdamu, na ulikuja chini kwa bkurithi katika namna ifuatayo:

42 Kutoka Adamu hadi aSethi, ambaye alitawazwa na Adamu akiwa na umri wa miaka sitini na tisa, na alibarikiwa naye miaka mitatu kabla ya kifo chake (cha Adamu), na kupokea ahadi ya Mungu kupitia baba yake, kwamba uzao wake watakuwa wateule wa Bwana, na kwamba kitahifadhiwa hadi mwisho wa dunia;

43 Kwa sababu yeye (Sethi) alikuwa mtu amkamilifu, na bufanano wake ulikuwa mfano halisi wa baba yake, kiasi kwamba alikuwa akionekana kama baba yake katika mambo yote, na aliweza kutofautiana naye tu kwa umri wake.

44 Enoshi alitawazwa katika umri wa miaka mia moja na thelathini na nne na miezi minne, kwa mkono wa Adamu.

45 Mungu akamtokea Kenani nyikani katika mwaka wa arobaini wa umri wake; naye alikutana na Adamu akisafiri kwenda mahali paitwapo Shedolamak. Alikuwa na miaka themanini na saba wakati alipopata kutawazwa.

46 Mahalaleli alikuwa na umri wa miaka mia nne na tisini na sita na siku saba wakati alipotawazwa kwa mkono wa Adamu, ambaye pia alimbariki.

47 Yaredi alikuwa na umri wa miaka mia mbili wakati alipotawazwa chini ya mkono wa Adamu, ambaye pia alimbariki.

48 aHenoko alikuwa na umri wa miaka ishirini na tano wakati alipotawazwa chini ya mkono wa Adamu; na alikuwa na miaka sitini na tano Adamu alipombariki.

49 Na yeye alimwona Bwana, na alitembea pamoja naye, na daima alikuwa mbele ya uso wake; na aalitembea pamoja na Mungu miaka mia tatu na sitini na mitano, ikimfanya kuwa na umri wa miaka mia nne na thelathini wakati balipohamishwa.

50 aMethusela alikuwa na umri wa miaka mia moja wakati alipotawazwa chini ya mkono wa Adamu.

51 Lameki alikuwa na umri wa miaka thelathini na mbili wakati alipotawazwa chini ya mkono wa Sethi.

52 aNuhu alikuwa na umri wa miaka kumi wakati alipotawazwa chini ya mkono wa Methusela.

53 Miaka mitatu kabla ya kifo cha Adamu, alimwita Sethi, Enoshi, Kenani, Mahalaleli, Yaredi, Henoko, na Methusela, ambao wote walikuwa amakuhani wakuu, pamoja na mabaki ya uzao wake waliokuwa wenye haki, katika bonde la bAdamu-ondi-Amani, na huko akawawekea juu yao baraka zake za mwisho.

54 Na Bwana akawatokea, nao wakainuka na kumbariki aAdamu, na wakamwita bMikaeli, mtawala, malaika mkuu.

55 Na Bwana akamfariji Adamu, na akamwambia: Nimekuweka wewe kuwa kiongozi; wingi wa mataifa utatoka kwako, na wewe utakuwa amtawala juu yao milele.

56 Na Adamu alisimama katikati ya makutano; na, licha ya kuwa alikuwa amepinda mgongo kwa sababu ya uzee, akiwa amejawa na Roho Mtakatifu, aalitabiri yale yote yatakayoupata uzao wake hata kizazi cha mwisho.

57 Mambo haya yote yaliandikwa katika kitabu cha Henoko, nayo yatashuhudiwa kwa wakati wake.

58 Ni kazi ya aMitume Kumi na Wawili, pia, bkuwatawaza na kuwapanga viongozi wengine wote wa kanisa, sawa sawa na ufunuo usemao:

59 Kwa kanisa la Kristo katika nchi ya Sayuni, katika nyongeza kwa asheria za kanisa kuhusu shughuli za kanisa—

60 Amini, ninawaambia, asema Bwana wa Majeshi, hapana budi kuwepo na awazee viongozi wa kuongoza juu ya wale walio katika ofisi ya mzee;

61 Na pia amakuhani kuongoza juu ya wale walio katika ofisi ya kuhani;

62 Na pia walimu akuongoza juu ya wale walio katika ofisi ya mwalimu, vile vile, na pia mashemasi—

63 Kwa hiyo, kutoka shemasi hadi mwalimu, na kutoka mwalimu hadi kuhani, na kutoka kuhani hadi mzee, kila mmoja kama wanavyoteuliwa, kulingana na maagano na amri za kanisa.

64 Halafu unakuja Ukuhani Mkuu, ambao ni mkubwa kuliko wote.

65 Kwa hiyo, ni muhimu kwamba mtu mmoja wa Ukuhani Mkuu ateuliwe kuusimamia Ukuhani, naye ataitwa Rais wa Ukuhani Mkuu wa Kanisa;

66 Au, katika maneno mengine, Kuhani Mkuu aKiongozi wa Ukuhani Mkuu wa Kanisa.

67 Kutoka kwa huyo kunakuja kusimamia ibada na baraka juu ya kanisa, kwa akuwekea mikono.

68 Kwa hiyo, ofisi ya askofu siyo sawa na hii; kwani aofisi ya askofu ni ya kusimamia mambo yote ya kimwili;

69 Hata hivyo, askofu lazima achaguliwe kutoka kwenye aUkuhani Mkuu, isipokuwa ni wa buzao halisi wa Haruni;

70 Kwani kama yeye siyo wa uzao halisi wa Haruni hawezi kushikilia funguo za ukuhani huo.

71 Hata hivyo, kuhani mkuu, ambaye, ni kwa mfano wa Melkizedeki, anaweza kuwekwa rasmi kwa ajili ya kusimamia mambo ya kimwili, akiwa mwenye maarifa juu yake kwa njia ya Roho wa kweli;

72 Na pia kuwa amwamuzi katika Israeli, kufanya shughuli za kanisa, kukaa katika hukumu juu ya wavunja sheria kulingana na ushuhuda kama utakavyo wekwa mbele yake kulingana na sheria, kwa msaada wa washauri wake, ambao amewachagua au atakao wachagua miongoni mwa wazee wa kanisa.

73 Hii ni kazi ya askofu ambaye siyo wa uzao halisi wa Haruni, bali ametawazwa kwenye Ukuhani huu Mkuu kwa mfano wa Melkizedeki.

74 Hivyo ndivyo atakuwa mwamuzi, hata mwamuzi wa wote miongoni mwa wakazi wa Sayuni, au katika vigingi vya Sayuni, au katika tawi lolote la kanisa ambapo atawekwa rasmi kwa huduma hii, hadi mipaka ya Sayuni ipanuliwe na ni muhimu kuwa na maaskofu au waamuzi wengine katika Sayuni au popote kwingineko.

75 Na ilimradi kuna maaskofu wengine walioteuliwa nao watafanya kazi katika ofisi hiyo hiyo.

76 Lakini mzaliwa halisi wa uzao wa Haruni anayo haki ya urais wa ukuhani huu, haki ya afunguo za huduma hii, kutenda kazi katika ofisi ya askofu pekee yake, bila washauri, isipokuwa katika shauri ambalo Rais wa Ukuhani Mkuu, kwa mfano wa Melkizedeki, anashtakiwa, kuwa kama mwamuzi katika Israeli.

77 Na uamuzi wa baraza lolote kati ya haya, ukubaliane na amri isemayo:

78 Tena, amini, ninawaambia, shughuli ya kanisa iliyo muhimu zaidi, na mashauri ya kanisa, yaliyo amagumu zaidi, kama hakuna kuridhika juu ya uamuzi wa askofu au waamuzi, yakabidhiwe na yapelekwe kwa baraza la kanisa, mbele ya bUrais wa Ukuhani Mkuu.

79 Na Urais wa baraza la Ukuhani Mkuu utakuwa na uwezo wa kuwaita makuhani wakuu wengine, hata kumi na wawili, kusaidia kama washauri; na hivyo Urais wa Ukuhani Mkuu na washauri wake watakuwa na uwezo wa kuamua juu ya ushuhuda kulingana na sheria za kanisa.

80 Na baada ya uamuzi huu lisiletwe tena kwenye kumbukumbu mbele ya Bwana; kwani hili ndilo baraza la juu kabisa la kanisa la Mungu, na ni uamuzi wa mwisho juu ya mabishano katika mambo ya kiroho.

81 Hakuna mtu yeyote aliye wa kanisa ambaye hahukumiwi na baraza hili la kanisa.

82 Na kadiri Rais wa Ukuhani Mkuu atakavyovunja sheria, ataletwa mbele ya baraza kuu la kanisa, ambalo litasaidiwa na washauri kumi na wawili wa Ukuhani Mkuu;

83 Na uamuzi wao juu ya kichwa chake utakuwa ndiyo mwisho wa mabishano juu yake.

84 Hivyo, hakuna atakaye samehewa kutokana na ahaki na sheria za Mungu, ili mambo yote yapate kufanyika katika utaratibu na katika ibada mbele zake, kulingana na kweli na haki.

85 Na tena, amini ninawaambia, kazi ya rais wa ofisi ya ashemasi ni kuwaongoza mashemasi kumi na wawili, kukaa katika baraza pamoja nao, na bkuwafundisha wajibu wao, wakijengana wao kwa wao, kama ilivyotolewa kulingana na maagano.

86 Na pia kazi ya rais juu ya ofisi ya awalimu ni kuwaongoza walimu ishirini na wanne, na kukaa katika baraza pamoja nao, kuwafundisha wajibu wa ofisi zao, kama ulivyotolewa katika maagano.

87 Pia kazi ya rais juu ya Ukuhani wa Haruni ni kuwaongoza amakuhani arobaini na wanane, na kukaa katika baraza pamoja nao, kuwafundisha wajibu wa ofisi zao, kama ulivyotolewa katika maagano—

88 Rais huyu anapaswa kuwa aaskofu; kwani hii ni mojawapo ya kazi za ukuhani huu.

89 Tena, kazi ya rais juu ya ofisi ya awazee ni kuwaongoza wazee tisini na sita, na kukaa katika baraza pamoja nao, na kuwafundisha kulingana na maagano.

90 Urais huu ni tofauti na ule wa sabini, na umedhamiriwa kwa wale ambao ahawasafiri ulimwenguni kote.

91 Na tena, kazi ya Rais wa ofisi ya Ukuhani Mkuu ni akuliongoza kanisa lote, na kuwa kama bMusa

92 Tazama, hii ndiyo hekima; ndiyo, kuwa amwonaji, bmfunuzi, mfasiri, na cnabii, akiwa na dvipawa vyote vya Mungu ambavyo huviweka juu ya kiongozi wa kanisa.

93 Na ni kulingana na ono lionyeshalo mpangilio wa aSabini, kwamba wanapaswa kuwa na marais saba wakiwaongoza, walioteuliwa kutoka katika idadi ya hao sabini;

94 Na rais wa saba kati ya marais hawa atawaongoza sita;

95 Na marais hawa saba watawachagua sabini wengine licha ya sabini wa kwanza ambao humo nao wanatoka, na watawaongoza hao;

96 Na pia sabini wengine, hadi saba mara sabini, kama kazi katika shamba la mizabibu litahitaji hivyo.

97 Na hawa sabini watakuwa awahudumu wa kusafiri, kwa Wayunani kwanza na pia kwa Wayahudi.

98 Kinyume chake maofisa wengine wa kanisa, ambao siyo wale Kumi na Wawili, wala Sabini, hawako chini ya wajibu wa kusafiri miongoni mwa mataifa yote, ila watasafiri kadiri hali zao zitakavyowaruhusu, licha ya kwamba wanaweza kuwa wanashikilia nafasi ya juu na ofisi zenye wajibu mkubwa katika kanisa.

99 Kwa sababu hiyo, sasa acha kila mtu na ajifunze awajibu wake, na kutenda kazi katika ofisi ambayo ameteuliwa, kwa bbidii yote.

100 Yule aliye amvivu hatahesabika kuwa mwenye bkustahili kusimama, na yule asiye jifunza wajibu wake na asiyeweza kujithibitisha yeye mwenyewe hatahesabika kuwa mwenye kustahili kusimama. Hivyo ndivyo. Amina.