Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 119


Sehemu ya 119

Ufunuo uliotolewa kupitia Joseph Smith Nabii, huko Far West, Missouri, 8 Julai 1838, katika jibu la ombi lake: “Ee Bwana! Onyesha kwa watumishi wako ni kiasi gani cha mali wataka kutoka kwa watu wako kwa ajili ya zaka.” Sheria ya zaka, kama inavyofahamika leo, haikuwa imetolewa kwa kanisa kabla ya ufunuo huu. Neno zaka katika sala ambayo imenukuliwa punde na katika mafunuo yaliyopita (64:23; 85:3; 97:11) haikumaanisha tu sehemu moja ya kumi, bali sadaka za hiari, au michango, kwenye mfuko wa Kanisa. Bwana awali alikuwa ametoa sheria kwa Kanisa sheria ya kuweka wakfu na usimamizi wa mali, ambazo waumini (hususani wazee viongozi) waliingia kwa agano ambalo lisingekuwa na mwisho. Kwa sababu ya kushindwa kwa wengi wao kuishi kulingana na agano hili, Bwana aliliondoa kwa muda na badala yake akatoa sheria ya zaka kwa Kanisa lote. Nabii alimwuliza Bwana ni kiasi gani cha mali yao Yeye alikitaka kwa madhumuni yake matakatifu. Jibu lilikuwa ufunuo huu.

1–5, Watakatifu wanapaswa kulipa mali yao ya ziada na halafu kutoa, kama zaka, sehemu moja ya kumi ya mapato yao kila mwaka; 6–7, Utaratibu huu utaitakasa nchi ya Sayuni.

1 Amini, hivyo ndivyo asemavyo Bwana, ninataka mali yao yote ya aziada iwekwe mikononi mwa askofu wa kanisa langu katika Sayuni,

2 Kwa ajili ya ujenzi wa anyumba yangu, na kwa ajili ya kuweka msingi wa Sayuni na kwa ajili ya ukuhani, na kwa ajili ya madeni ya Urais wa Kanisa langu.

3 Na huu ndiyo utakuwa mwanzo wa kulipa azaka kwa watu wangu.

4 Na baada ya hiyo, kwa wale ambao kwa jinsi hiyo wamelipa zaka watalipa sehemu moja ya kumi ya mapato yao ya kila mwaka; na hii itakuwa sheria ya kudumu kwao milele, kwa ajili ya ukuhani wangu mtakatifu, asema Bwana.

5 Amini ninawaambia, itakuwa kwamba wale wote wakusanyikao katika nchi ya aSayuni watalipishwa zaka ya mali zao za ziada, nao watatii sheria hii, au la sivyo wataonekana hawastahili kukaa miongoni mwenu.

6 Na ninawaambia, kama watu wangu hawatatii sheria hii, kuishika kitakatifu, na kwa sheria hii wakanitakasia nchi ya aSayuni, ili sheria zangu na hukumu zangu zipate kushikwa juu yake, ili ipate kuwa takatifu zaidi, tazama, amini ninawaambia, haitakuwa nchi ya Sayuni kwenu ninyi.

7 Na huu ndiyo utakuwa utaratibu kwa avigingi vyote vya Sayuni. Hivyo ndivyo. Amina.