Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 46


Sehemu ya 46

Ufunuo uliotolewa kupitia Joseph Smith Nabii kwa Kanisa, huko Kirtland, Ohio, 8 Machi 1831. Katika wakati huu wa mwanzo wa Kanisa, mpangilio wa aina moja wa kuendesha ibada za Kanisa ulikuwa bado hujaanzishwa. Hata hivyo, desturi ya kuwaruhusu waumini pekee na wachunguzi wa dhati wa Kanisa kwenye mikutano ya Sakramenti na mikutano mingine ya Kanisa limekuwa jambo la kawaida. Ufunuo huu unaonyesha mapenzi ya Bwana juu ya kuongoza na kuendesha mikutano na mwongozo Wake juu ya kutafuta na kutambua vipawa vya Roho.

1–2, Wazee wataendesha mikutano kama watakavyoongozwa na Roho Mtakatifu; 3–6, Watafuta ukweli yapaswa wasitengwe kwenye ibada za sakramenti; 7–12, Mwombeni Mungu na tafuteni vipawa vya Roho; 13–26, Hesabu ya baadhi ya vipawa hivyo yatolewa; 27–33, Viongozi wa Kanisa wamepewa uwezo wa kutambua vipawa vya Roho.

1 Sikilizeni, Enyi watu wa kanisa langu; kwani amini ninawaambia kwamba mambo haya yalizungumzwa kwa amanufaa na mafundisho yenu.

2 Lakini licha ya mambo yale ambayo yameandikwa, daima imekuwa ikitolewa kwa awazee wa kanisa langu kutoka mwanzo, na daima itakuwa hivyo, bkuendesha mikutano yote kama inavyoelekezwa na kuongozwa na Roho Mtakatifu.

3 Hata hivyo mnaamriwa kamwe amsimtupe yeyote nje ya mikutano yenu ya jumuiya, ambayo hufanyika mbele ya walimwengu.

4 Pia mnaamriwa msimtupe yeyote aliye wa akanisa nje ya mikutano yenu ya sakramenti; hata hivyo, kama kuna yeyote aliyekosa, acheni basipokee hadi atakapofanya suluhu.

5 Na tena ninawaambia, hamtamtupa yeyote nje ya mikutano yenu ya sakramenti ambaye anautafuta ufalme kwa dhati—ninalisema hili juu ya wale ambao si wa kanisa.

6 Na tena ninawaambia, juu ya amikutano yenu ya uthibitisho, kwamba endapo kutakuwa na yeyote ambaye si wa kanisa, ambaye huutafuta ufalme kwa dhati, msimtupe nje.

7 Lakini mnaamriwa katika mambo yote akumwomba Mungu, awapaye kwa ukarimu, na kile ambacho Roho hushuhudia kwenu hata hivyo nataka ninyi mkifanye katika butakatifu wote wa moyo, mkitembea wima mbele zangu, cmkifikiria mwisho wa wokovu wenu, mkifanya mambo yote kwa sala na dshukrani, ili msiweze ekudanganywa na pepo wachafu, na mafundisho ya fmaibilisi, au gamri za wanadamu; kwani baadhi ni za wanadamu na nyingine za mapepo.

8 Kwa hivyo, kuweni waangalifu msije kudanganywa; na ili msidanganywe atakeni sana karama zilizo kuu, daima mkikumbuka ni kwa nini zinatolewa;

9 Kwani amini ninawaambia, hutolewa kwa manufaa ya wale ambao hunipenda Mimi na hushika amri zangu zote, na yule atafutaye kufanya haya; ili wote waweze kufaidika wale wanitafutao au kuniomba, kwamba wanaomba na hawaombi kwa aishara ili wapate bkuvitumia kwa tamaa zao.

10 Na tena, amini ninawaambia, ningetaka kwamba daima mkumbuke, na daima yawekeni katika aakili zenu bvipawa hivyo ni vipi, ambavyo hutolewa kwa kanisa.

11 Kwani wote hawapokei vipawa vyote; kwani kuna vipawa vingi, na kwa akila mtu kipawa kimetolewa na Roho wa Mungu.

12 Kwa wengine wamepewa kimoja, na wengine wamepewa kingine, ili wote waweze kufaidika.

13 Kwa wengine kinatolewa na Roho Mtakatifu akujua kwamba Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu, na kwamba alisulubiwa kwa ajili ya dhambi za ulimwengu.

14 Kwa wengine kimetolewa akuamini juu ya maneno yao, ili hao pia waweze kuwa na uzima wa milele kama wataendelea kuwa waaminifu.

15 Na tena, kwa wengine imetolewa na Roho Mtakatifu kujua atofauti za huduma, kama itakavyo mpendeza Bwana yeye yule, kulingana na matakwa ya Bwana, akilinganisha rehema zake kulingana na hali za wanadamu.

16 Na tena, hutolewa na Roho Mtakatifu kwa wengine kujua tofauti za kutenda kazi, kama ni za Mungu, kwamba mafunuo hayo ya Roho yaweze kutolewa kwa kila mtu kwa faida ya wote.

17 Na tena, amini ninawaambia, kwa mwingine amepewa na Roho wa Mungu, neno la ahekima.

18 Kwa mwingine neno la amaarifa, ili wote waweze kufundishwa kuwa wenye hekima na kuwa na maarifa.

19 Na tena kwa wengine wamepewa kuwa na aimani ya kuponywa;

20 Na wengine wamepewa kuwa na imani ya akuponya.

21 Na tena, kwa wengine wamepewa kufanya amiujiza;

22 Na kwa wengine wamepewa akutoa unabii;

23 Na kwa wengine akuzitambua roho.

24 Na tena, wengine wamepewa kunena kwa alugha;

25 Na mwingine amepewa tafsiri ya lugha.

26 Na avipawa hivi vyote hutoka kwa Mungu, kwa manufaa ya bwatoto wa Mungu.

27 Na kwa aaskofu wa kanisa, na kwa watu wa aina hiyo ambao Mungu atawateua na kuwatawaza kulisimamia kanisa na kuwa wazee wa kanisa, watapewa bkuvitambua vipawa hivyo vyote isije pakawepo mtu miongoni mwenu akitabiri na wala isiwe kutoka kwa Mungu.

28 Na itakuwa kwamba yule aombaye katika aRoho atapokea katika Roho;

29 Kwamba baadhi waweza kupewa kuwa na vipawa vyote, ili paweze kuwa na kiongozi, ili kwamba kila muumini aweze kufaidika navyo.

30 Yule ambaye aanaomba katika bRoho aomba kulingana na cmapenzi ya Mungu; kwa sababu hiyo hufanyika kwake kama aombavyo.

31 Na tena, ninawaambia, mambo yote lazima yafanyike katika jina la Kristo, lolote mfanyalo katika Roho;

32 Na ni lazima mtoe ashukrani kwa Mungu katika Roho kwa baraka zozote mbarikiwazo.

33 Na ni lazima mtende awema na butakatifu mbele zangu daima. Hivyo ndivyo. Amina.