Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 93


Sehemu ya 93

Ufunuo uliotolewa kupitia Joseph Smith Nabii, huko Kirtland, Ohio, 6 Mei 1833.

1–5, Wote walio waaminifu watamwona Bwana; 6–18, Yohana anashuhudia kuwa Mwana wa Mungu alikwenda neema hadi neema mpaka yeye akapokea utimilifu wa utukufu wa Baba; 19–20, Watu waaminifu, wanaokwenda neema hadi neema, pia nao watapata utimilifu Wake; 21–22, Wale walio wazaliwa kupitia Kristo ndiyo Kanisa la Mzaliwa wa Kwanza; 23–28, Kristo alipokea utimilifu wa ukweli wote, na mwanadamu kwa utii anaweza kufanya vivyo hivyo; 29–32, Mwanadamu mwanzoni alikuwa pamoja na Mungu; 33–35, Vitu vya asili ni vya milele, na mwanadamu aweza kupokea utimilifu wa furaha shangwe katika Ufufuko; 36–37, Utukufu wa Mungu ni akili; 38–40, Watoto hawana hatia mbele za Mungu kwa sababu ya ukombozi wa Kristo; 41–53, Ndugu viongozi wanaamriwa kuziweka sawa sawa familia zao.

1 Amini, hivyo ndivyo asemavyo Bwana: Itakuwa kwamba kila mtu aatakayeziacha dhambi zake na kuja kwangu, na bkulilingana jina langu, na ckuitii sauti yangu, na kushika amri zangu, datauona euso wangu na kujua kuwa Mimi ndiye;

2 Na kuwa Mimi ni anuru ya kweli imwangazayo kila mtu ajaye ulimwenguni;

3 Na kuwa Mimi ni andani ya Baba, na Baba yu ndani yangu, na kuwa Baba na Mimi tu wamoja—

4 Baba kwa asababu bamenipa Mimi utimilifu wake, na Mwana kwa sababu nilikuwepo ulimwenguni na kufanya cmwili kuwa hema takatifu yangu, na kuishi miongoni mwa wanadamu.

5 Nami nilikuwa ulimwenguni na nikapokea ya Baba yangu, na akazi zake zikadhihirika wazi.

6 Na aYohana aliona na kushuhudia utimilifu wa butukufu wangu, na utimilifu wa ushuhuda wa cYohana utafunuliwa hapo baadaye.

7 Na alitoa ushuhuda, akisema: Niliuona utukufu wake, kwamba alikuwepo hapo amwanzo, kabla ya ulimwengu kuwepo;

8 Kwa hiyo, hapo mwanzo aNeno alikuwepo, kwani alikuwa Neno, hata mjumbe wa wokovu—

9 aNuru na bMkombozi wa ulimwengu; Roho wa kweli, aliyekuja ulimwenguni, kwa sababu ulimwengu uliumbwa naye, na ndani yake mlikuwa na uzima wa wanadamu na nuru ya wanadamu.

10 Dunia aziliumbwa naye; wanadamu waliumbwa naye; vitu vyote viliumbwa naye, na kwa njia yake, na kutoka kwake.

11 Na mimi, Yohana, ninashuhudia kwamba niliuona utukufu wake, kama utukufu wa Mzaliwa Pekee wa Baba, amejaa neema na kweli, hata Roho wa kweli, ambaye alikuja na akakaa katika mwili, na akakaa miongoni mwetu.

12 Na mimi Yohana, niliona kwamba hakupokea autimilifu mwanzoni, bali alipokea bneema juu ya neema;

13 Naye hakupokea utimilifu mwanzoni, bali aliendelea kutoka aneema hadi neema, mpaka akapokea utimilifu;

14 Na hivyo akaitwa aMwana wa Mungu, kwa sababu hakuwa amepokea utimilifu mwanzoni.

15 Na mimi, aYohana, ninashuhudia, na lo, mbingu zikafunguka, na bRoho Mtakatifu akashuka juu yake katika umbo la cnjiwa, na akatua juu yake, na hapo ikaja sauti kutoka mbinguni ikisema: Huyu ni dMwanangu Mpendwa.

16 Na mimi, Yohana, ninashuhudia kwamba alipata utimilifu wa utukufu wa Baba;

17 Na akapokea auwezo bwote, kote mbinguni na duniani, na utukufu wa cBaba ulikuwa pamoja naye, kwa kuwa alikaa ndani yake.

18 Na itakuwa, kwamba kama ni waaminifu mtapokea utimilifu wa ushuhuda wa Yohana.

19 Ninayatoa kwenu ninyi maneno haya ili muweze kufahamu na kujua namna ya akuabudu, na kujua nini mnachokiabudu, ili muweze kuja kwa Baba katika jina langu, na kwa wakati wake mpokee utimilifu wake.

20 Kwani ikiwa mnazishika aamri zangu mtaupokea butimilifu wake, na ckutukuzwa ndani yangu, kama Mimi ndani ya Baba; kwa hiyo, ninawaambia, mtapokea dneema juu ya neema.

21 Na sasa, amini ninawaambia, hapo amwanzo nilikuwepo kwa Baba, na Mimi ndiye bMzaliwa wa Kwanza;

22 Na wale wote walio wazaliwa kupitia mimi ni awashiriki wa butukufu huo huo, na ndiyo kanisa la Mzaliwa wa Kwanza.

23 Ninyi pia mlikuwepo mwanzoni apamoja na Baba; kile ambacho ni Roho, hata Roho wa kweli;

24 Na aukweli ni bmaarifa ya mambo kama yalivyo, na kama yalivyokuwa, na kama yatakavyokuwa;

25 Na chochote kilicho azaidi au pungufu ya hivi ni roho wa yule mwovu ambaye alikuwa bmuongo kutoka mwanzo.

26 Roho wa akweli huyo ndiye wa Mungu. Mimi ni Roho wa kweli, na Yohana alitoa ushuhuda juu yangu, akisema: Alipokea utimilifu wa kweli, ndiyo, hata kweli yote;

27 Na hakuna mtu apokeaye autimilifu isipokuwa amezishika amri zake.

28 Yule aazishikaye amri zake hupokea kweli na bnuru, hadi ametukuzwa katika kweli na ckujua mambo yote.

29 Mwanadamu pia amwanzoni alikuwa na Mungu. bAkili, au nuru ya kweli, haikuumbwa au kutengenezwa, na wala kamwe haiwezekani kuwa.

30 Kweli yote ni huru katika mazingira yale ambayo Mungu ameiweka, ili akujiamulia yenyewe, kama akili yote pia; vinginevyo hakuna maisha.

31 Tazama, hapa ndipo ilipo ahaki ya kujiamulia ya mwanadamu, na hapa ndipo ilipo hukumu ya mwanadamu; kwa sababu kile kilichokuwepo kutoka mwanzoni kinajitokeza bwazi kwao, nao hawaipokei nuru.

32 Na kila mtu ambaye roho yake haiipokei anuru iko chini ya hukumu.

33 Kwani mwanadamu ni aroho. bVitu vya asili ni vya milele, na roho na vitu vya asili, ambavyo vimeungana na haviwezi kutenganishwa, hupokea shangwe kamilifu;

34 Na avikitenganishwa, mwanadamu hawezi kupokea bshangwe kamilifu.

35 aVitu vya asili ni hema takatifu ya Mungu; ndiyo, mwanadamu ni hema takatifu ya Mungu, mahekalu, hata bmahekalu; na lolote likichafuliwa, Mungu ataliharibu hekalu hilo.

36 aUtukufu wa Mungu ni bakili, au, kwa maneno mengine, cnuru na kweli.

37 Nuru na kweli humkataa yule amwovu.

38 Kila roho ya mwanadamu ahaikuwa na dhambi hapo mwanzoni; na Mungu akiwa amekwisha bmkomboa mwanadamu kutokana na canguko, wanadamu wakaja tena, katika hali yao ya uchanga, wakiwa dsafi mbele za Mungu.

39 Na yule mwovu huja na akuziondoa nuru na kweli, kwa kutotii, kutoka kwa wanadamu, na kwa sababu ya bmapokeo ya baba zao.

40 Lakini nimewaamuru ninyi kuwalea awatoto wenu katika nuru na kweli.

41 Lakini amini ninakuambia, mtumishi wangu Frederick G. Williams, umekaa katika hatia hii;

42 aHujawafundisha watoto wako nuru na kweli, kulingana na amri; na yule mwovu bado anazo nguvu juu yako, na hii ndiyo chanzo cha mateso yako.

43 Na sasa amri ninaitoa kwako—kama utakombolewa utaiweka asawa sawa nyumba yako mwenyewe, kwani kuna mambo mengi yasiyo sawa katika nyumba yako.

44 Amini, ninakuambia wewe mtumishi wangu Sidney Rigdon, kuwa katika baadhi ya mambo hajashika amri kuhusiana na watoto wake; kwa hiyo, kwanza uirekebishe nyumba yako.

45 Amini, ninamwambia mtumishi wangu Joseph Smith, Mdogo, au katika maneno mengine, nitawaita ninyi amarafiki, kwa kuwa ninyi ni marafiki zangu, na mtapata urithi pamoja nami—

46 Niliwaita, ninyi awatumishi kwa faida ya ulimwengu, na ninyi ni watumishi wao kwa faida yangu—

47 Na sasa, amini ninamwambia Joseph Smith, Mdogo—Hujashika amri, na inakulazimu aukemewe mbele za Bwana;

48 aFamilia yako lazima itubu na kuacha baadhi ya mambo, na kuyasikiliza kwa makini maneno yako, au, wataondoshwa kwenye nafasi yao.

49 Nisemacho kwa mmoja ninasema kwa wote; aombeni daima asije yule mwovu akawa na nguvu ndani yenu, na kuwaondosha kwenye nafasi yenu.

50 Pia mtumishi wangu Newel K. Whitney, askofu wa kanisa langu, inafaa akemewe, na kuirekebisha nyumba yake, na kuona kuwa wanakuwa na bidii na wenye kujali nyumbani, na kuomba daima, au vinginevyo wataondoshwa kwenye anafasi yao.

51 Sasa, ninawaambia marafiki zangu, na mtumishi wangu Sidney Rigdon aende safari yake, na afanye haraka, na pia akitangaza mwaka auliokubaliwa wa Bwana, na injili ya wokovu, vile nitakavyompa kunena; na kwa sala yenu ya imani kwa nia moja nitamsaidia.

52 Na watumishi wangu Joseph Smith, Mdogo, na Frederick G. Williams wafanye upesi pia, nao watapewa kulingana na sala ya imani; na kadiri mtakavyoshika maneno yangu hamtashindwa katika ulimwengu huu, wala katika ulimwengu ujao.

53 Na, amini ninawaambia, kwamba ni mapenzi yangu kuwa mfanye upesi akutafsiri maandiko yangu, na bkupata cmaarifa ya historia, na ya mataifa, na ya falme, ya sheria za Mungu na mwanadamu, na hii yote ni kwa ajili ya wokovu wa Sayuni. Amina.