Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 48


Sehemu ya 48

Ufunuo uliotolewa kupitia Joseph Smith, Nabii, huko Kirtland, Ohio, 10 Machi 1831. Nabii alimwuliza Bwana juu ya utaratibu wa kutumia katika kununua ardhi kwa ajili ya makazi ya watakatifu. Hili lilikuwa ni jambo muhimu katika suala la uhamaji wa waumini wa Kanisa kutoka majimbo ya mashariki ya Marekani, katika utii kwa amri ya Bwana kwamba iliwapasa kukusanyika Ohio (ona sehemu ya 37:1–3; 45:64).

1–3, Watakatifu wa Ohio washirikiane ardhi yao pamoja na ndugu zao; 4–6, Watakatifu wanunue ardhi, waujenge mji, na wafuate ushauri wa viongozi wao.

1 Ni muhimu kwa wakati huu kubaki katika mahali penu mnapoishi, ilimradi kwamba hali hiyo ni vizuri kwenu.

2 Na ikiwa mnayo ardhi, amtaitoa kwa ndugu zenu wa mashariki;

3 Na ikiwa hakuna ardhi na wainunue kwa wakati huu katika maeneo yale yaliyo karibu, kama itakavyowapendeza wao, kwani ni lazima na ni muhimu kwamba wapate mahali pa kuishi kwa wakati huu.

4 Ni muhimu kwenu kujiwekea akiba ya fedha kadiri inavyowezekana, na kuwa jipatieni kila kitu kwa haki, ili wakati ukifika muweze akujinunulia ardhi kwa kujenga mji na Ni muhimu kwenu kujiwekea akiba ya fedha kadiri inavyowezekana, na kuwa jipatieni kila kitu kwa haki, ili wakati ukifika muweze bkujinunulia ardhi kwa kujenga mji na hata kwa urithi wenu.

5 Mahali bado hapajafunuliwa; lakini baada ya kuwasili ndugu zenu kutoka mashariki watachaguliwa awatu fulani, nao watapewa bkujua mahali hapo, au patafunuliwa kwao.

6 Na hao watachaguliwa ili kununua ardhi, na kuweka msingi wa amji; na ndipo mtaanza kukusanyika pamoja na familia zenu, kila mtu kulingana na bfamilia yake, na kwa kadiri ya hali yake, na kadiri atakavyoelezwa na urais na askofu wa kanisa, kulingana na sheria na amri ambazo mmezipokea, na ambazo mtazipokea baadaye. Hivyo ndivyo. Amina.