Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 50


Sehemu ya 50

Ufunuo uliotolewa kupitia Joseph Smith Nabii, huko Kirtland, Ohio, 9 Mei 1831. Historia ya Joseph Smith inaeleza kwamba baadhi ya wazee walikuwa hawaelewi kujitokeza kwa roho tofauti zilizoenea katika nchi na kwamba ufunuo huu ulitolewa kama jibu kwa maulizo yake maalumu juu ya jambo hili. Yaliyokuwa yakiitwa matukio ya kiroho wala hayakuwa mageni miongoni mwa waumini, baadhi yao walikuwa wakidai kupokea maono na mafunuo.

1–5, Roho nyingi za uongo zimeenea katika nchi; 6–9, Ole wao wanafiki na wale waliotengwa na Kanisa; 10–14, Wazee watahubiri injili kwa Roho; 15–22, Wote mhubiri na msikilizaji wanahitaji kuangaziwa na Roho; 23–25, Kile kisichojenga siyo cha Mungu; 26–28, Waaminifu ni wamiliki wa vitu vyote; 29–36, Sala za walio safi hujibiwa; 37–46, Kristo ndiye Mchungaji Mwema na Jiwe la Israeli.

1 Sikilizeni, Enyi wazee wa kanisa langu, na itegeeni sikio sauti ya Mungu aliye hai; na litilieni maanani neno la hekima ambalo litatolewa kwenu, kulingana na vile mlivyoomba na kukubaliwa juu ya kanisa, na roho ambazo zimeenea katika nchi.

2 Tazama, amini ninawaambia, kwamba kuna roho nyingi ambazo ni aroho za uongo, ambazo zimeenea katika nchi, zikiudanganya ulimwengu.

3 Na pia aShetani ametafuta kuwadanganya ninyi, ili aweze kuwapindua.

4 Tazama, Mimi, Bwana, nimewaangalia, na nimeona machukizo katika kanisa ambalo ahulikiri jina langu.

5 Lakini wamebarikiwa wale walio waaminifu na wenye asubira, ikiwa katika kuishi au katika kifo, kwani wataurithi uzima wa milele.

6 Bali ole wao awadanganyifu na wanafiki, kwani, hivyo ndivyo asemavyo Bwana, nitawaleta kwenye hukumu.

7 Tazama, amini ninawaambia, kuna awanafiki miongoni mwenu, ambao wamewadanganya baadhi yenu, ambao wamempa bnguvu cadui; lakini wa daina hiyo wataokolewa;

8 Lakini wanafiki watatambulika na akukatiliwa mbali, iwe katika kuishi au katika kufa, kama vile mimi nitakavyo; na ole wao waliokatiliwa mbali kutoka kwenye kanisa langu, kwani wao ulimwengu umewashinda.

9 Kwa hiyo, acha kila mtu ajihadhari ili asije akafanya kile kisicho cha kweli na haki mbele zangu.

10 Na sasa njooni kwa njia ya Roho, asema Bwana, kwa wazee wa kanisa lake, na atusemezane, ili mpate kuelewa;

11 Na tusemezane kama vile watu wanavyosemezana mmoja kwa mwingine uso kwa uso.

12 Sasa, wakati watu wanaposemezana, huelewana, kwa sababu husemezana kama watu; hivyo ndivyo nitakavyo Mimi, Bwana, kusemezana nanyi ili kwamba muweze akunielewa.

13 Kwa hiyo, Mimi Bwana ninawauliza swali hili—ammetawazwa kwa lipi?

14 Kwa kuhubiri injili yangu kwa njia ya aRoho, hata bMfariji aliyetumwa kufundisha ukweli.

15 Nanyi mkapokea aroho nyingine ambazo hamkuweza kuzielewa, na mkazipokea kama ni za Mungu; na katika hili ninyi mnajiteteaje?

16 Tazama, mtajibu swali hili ninyi wenyewe; hata hivyo, nitakuwa mwenye huruma kwenu; yule aliye dhaifu miongoni mwenu atafanywa baadaye kuwa amwenye nguvu.

17 Amini ninawaambia, yule aliyetawazwa na mimi na kutumwa kwenda akulihubiri neno la kweli kwa njia ya Mfariji, katika Roho wa kweli, je, afundisha kwa bRoho wa kweli au kwa njia nyingine?

18 Na kama itakuwa kwa njia nyingine hatokani na Mungu.

19 Na tena, yule apokeaye neno la kweli, je, hulipokea kwa Roho wa kweli au kwa njia nyingine?

20 Kama ni kwa njia nyingine hatokani na Mungu.

21 Kwa hiyo, kwa nini kwamba hamwezi kuelewa na kujua, kwamba yule ambaye hulipokea neno kwa njia ya Roho wa kweli hulipokea kama vile lifundishwavyo na Roho wa kweli?

22 Kwa sababu hiyo, yule ambaye huhubiri na yule apokeaye, huelewana, na wote ahujengana na bkufurahi kwa pamoja.

23 Na kile kisichojenga siyo cha Mungu, nacho ni agiza.

24 Kile kilicho cha Mungu ni anuru; na yule ambaye huipokea nuru, na bkukaa ndani ya Mungu, hupokea cnuru zaidi; na nuru hiyo huzidi kungʼara hata mchana mkamilifu.

25 Na tena, amini ninawaambia, na ninalisema ili muweze kujua aukweli, ili muweze kuifukuza giza kutoka miongoni mwenu;

26 Yule aliyetawazwa na Mungu na kutumwa, huyo ndiye ameteuliwa kuwa amkuu, bila kujali kuwa yeye ni mdogo na bmtumishi wa wote.

27 Kwa hiyo, yeye ni ammiliki wa vitu vyote; kwani vitu vyote viko chini yake, kote mbinguni na duniani, uzima na nuru, Roho na bnguvu, ametumwa kwa mapenzi ya Baba kupitia Mwana wake, Yesu Kristo.

28 Lakini hakuna mwanadamu aliye mmiliki wa vitu vyote isipokuwa yule aliye atakaswa na bkuoshwa dhambi zote.

29 Na kama umetakaswa na kuoshwa kutokana na dhambi zote, autaomba kitu chochote utakacho katika jina la Yesu nalo litafanyika.

30 Lakini jueni hili, mtafunuliwa nini cha kuomba; na kama vile mlivyoteuliwa akuongoza, roho zitakuwa chini yenu.

31 Kwa hiyo, itakuja kutokea, kwamba kama utaona aroho amejitokeza ambaye huwezi kumwelewa, na wewe humpokei roho huyo, utamwuliza Baba katika jina la Yesu; na kama haitoi roho hiyo kwako, ndipo waweza kujua kwamba haitokani na Mungu.

32 Na utatolewa kwako, auwezo juu ya pepo hao; nawe utatangaza dhidi ya pepo huyo kwa sauti kubwa kama hatokani na Mungu—

33 Siyo kwa amashtaka ya kumlaumu, ili asije akakushinda, wala siyo kwa bkujisifu wala kufurahia, ili nawe usije ukakamatwa.

34 Yule ambaye hupokea vya Mungu, na avihesabu kuwa ni vya Mungu; na afurahi kwamba Mungu humhesabu kuwa mwenye kustahili kupokea.

35 Na kwa kutilia maanani na kuyatenda mambo haya ambayo mmeyapokea, na yale mtakayoyapokea—na aufalme mliopewa na Baba, na buwezo wa kuvishinda vitu vyote ambavyo yeye hakuvianzisha.

36 Na tazama, amini ninawaambia, mmebarikiwa ninyi ambao sasa mnayasikiliza maneno yangu kutoka kinywa cha mtumishi wangu, kwani ninyi ammesamehewa dhambi zenu.

37 Na mtumishi wangu Joseph Wakefield, ambaye napendezwa naye, na mtumishi wangu aParley P. Pratt waende miongoni mwa makanisa na kuyaimarisha kwa neno la bkufaa;

38 Na pia mtumishi wangu John Corrill, au na watumishi wangu wengi wengineo kama walivyotawazwa kwenye ofisi hii, na acheni wafanye kazi katika ashamba la mizabibu, na acheni mtu yeyote asiwazuie kufanya kile ambacho nimekiteua kwao—

39 Kwa hiyo, katika hili mtumishi wangu aEdward Partridge hasamehewi; isipokuwa atubu na atasamehewa.

40 Tazama, ninyi ni watoto wadogo na hamuwezi akuyastahimili yote hivi sasa; na lazima bmkue katika cneema na katika ujuzi wa dukweli.

41 aMsiogope, ninyi bwatoto wadogo, kwani ninyi ni wangu, na Mimi cnimeushinda ulimwengu, nanyi ndiyo wale ambao Baba dalinipa;

42 Na hakuna hata mmoja wao wale ambao baba amenipatia aatakayepotea.

43 Na Baba na Mimi tu awamoja. Mimi ni ndani ya Baba na Baba yu ndani yangu; na kadiri ninyi mlivyonipokea Mimi, ninyi mu ndani yangu nami ni ndani yenu,

44 Kwa hivyo, Mimi nipo katikati yenu, na mimi ni amchungaji mwema, na bjiwe la Israeli. Yule ajengaye juu ya cmwamba huu dhataanguka kamwe.

45 Na siku yaja ambayo mtaisikia sauti yangu na akuniona, na kujua kwamba Mimi ndimi.

46 aKesheni basi, ili muweze kuwa btayari. Hivyo ndivyo. Amina.