Kitaswira, Yesu Kristo na injili Yake, ambao ndiyo msingi na msaada imara (M&M 11:24 ; 33:12–13 ). Mwamba pia waweza kumaanisha ufunuo, ambao kwa huo Mungu hufanya injili Yake ijulikane kwa wanadamu (Mt. 16:15–18 ).
Yeye ni mwamba, kazi yake ni kamilifu, Kum. 32:4 .
Bwana ni mwamba wangu; nitamwamini yeye, 2 Sam. 22:2–3 .
Jiwe likachongwa pasipo mikono, Dan. 2:34–35 .
Msingi wake ulijengwa juu ya mwamba, Mt. 7:25 (3Â Ne. 14:25 ).
Yesu Kristo ndiye jiwe lile ambalo lilidharauliwa, Mdo. 4:10–11 .
Mwamba ule ulikuwa Kristo, 1 Kor. 10:1–4 (Ku. 17:6 ).
Yule aliyejengwa juu ya mwamba huupokea ukweli, 2Â Ne. 28:28 .
Wayahudi watalikataa lile jiwe [Kristo] ambalo juu yake wangelijenga, Yak. (KM) 4:15–17 .
Ni juu ya mwamba wa Mkombozi wetu kwamba ni lazima tujenge msingi wetu, Hel. 5:12 .
Yeyote ajengaye juu ya mafundisho ya Kristo hujenga juu ya mwamba wake naye hataanguka wakati mafuriko yatakapokuja, 3 Ne. 11:39–40 (Mt. 7:24–27 ; 3 Ne. 18:12–13 ).
Mtu mwenye hekima alijenga nyumba yake juu ya mwamba, 3Â Ne. 14:24 .
Kama mmejengwa juu ya mwamba wangu, dunia na jehanamu hazitawashinda, M&M 6:34 .
Yule ajengaye juu ya mwamba huu hataanguka kamwe, M&M 50:44 .