Misaada ya Kujifunza
Omni


Omni

Mnefi mtunza kumbukumbu katika Kitabu cha Mormoni aliyeandika katika takribani mwaka wa 361 B.K. (Yar. 1:15; Omni 1:1–3).

Kitabu cha Omni

Kitabu kilichotafsiriwa kutoka katika mabamba madogo ya Nefi katika Kitabu cha Mormoni. Kitabu kina mlango mmoja tu, ambacho kina maelezo ya vita miongoni mwa Wanefi na Walamani. Omni aliandika mistari mitatu tu ya mwanzo ya kitabu hiki. Mabamba hayo kisha yakakabidhiwa kwa kupokezana kwa Amaroni, Kemisha, Abinadomu, na mwishowe Amaleki. Amaleki alikabidhi mabamba hayo kwa mfalme Benjamini, mfalme wa Zarahemla.