Katika maandiko, maskini yaweza kutumika kwa (1) watu ambao hawana vitu vya mahitaji muhimu, kama vile chakula, mavazi, na malazi, au (2) watu walio wanyenyekevu na wasio na kiburi.
Maskini katika mahitaji ya muhimu
Usimfumbie mkono wako nduguyo maskini, Kum. 15:7 .
Mwovu katika kiburi chake huwatesa walio maskini, Zab. 10:2 .
Mwenye kuwagawia maskini hatapungukiwa, Mit. 28:27 .
Walete maskini nyumbani kwako, Isa. 58:6–7 .
Ukitaka kuwa mkamilifu, wape maskini, Mt. 19:21 (Mk. 10:21 ; Lk. 18:22 ).
Je, Mungu hakuwachagua maskini wa ulimwengu huu, Yak. (Bib.) 2:5 .
Kwa sababu wao ni matajiri wanawadharau maskini, 2Â Ne. 9:30 .
Kupata msamaha wa dhambi zenu, wapeni maskini mali zenu, Mos. 4:26 .
Waligawa mali zao kwa maskini, Alma 1:27 .
Mkiwanyima wenye shida, sala zenu si kitu, Alma 34:28 .
Wanefi walikuwa na vitu vyote sawa baina yao; hapakuwa na maskini na tajiri, 4Â Ne. 1:3 .
Heri zaidi kwao wale wanaojinyenyekeza wenyewe pasipo kulazimishwa kwa sababu ya ufukara, Alma 32:4–6, 12–16 .
Heri maskini wa roho wajao kwangu, 3Â Ne. 12:3 (Mt. 5:3 ).