Kusema uongo Ona pia Danganya, Kudanganya, Udanganyifu; Kusema uovu; Mwaminifu, Uaminifu Taarifa yoyote yenye uongo au isiyo kweli kwa madhumuni ya kudanganya. Msiibe, wala msidanganye, wala msiambiane uongo, Law. 19:11. Ninauchukia uongo na umekithiri, Zab. 119:163. Midomo ya uongo ni chukizo kwa Bwana, Mit. 12:22. Ni watu wangu hao ambao hawatasema uongo, Isa. 63:8. Ibilisi ndiye mwongo na baba wa uongo, Yn. 8:44 (2 Ne. 2:18; Eth. 8:25; Musa 4:4). Hukumwambia uongo mwanadamu, bali Mungu, Mdo. 5:4 (Alma 12:3). Kama mtu akisema, Nampenda Mungu, naye anamchukia ndugu yake, yeye ni mwongo, 1 Yoh. 4:20. Waongo wote wanayo sehemu yao katika mauti ya pili, Ufu. 21:8 (M&M 63:17). Ole wako mwongo, kwani atatupwa chini jehanamu, 2 Ne. 9:34. Wengi watafundisha mafundisho ya uongo, wakisema: danganyeni kidogo na hakuna baya ndani yake, 2 Ne. 28:8–9 (M&M 10:25). Je, wadhani waweza kudanganya kwa Bwana, Alma 5:17. Wewe u Mungu wa ukweli nawe huwezi kudanganya, Eth. 3:12 (Hes. 23:19; 1 Sam. 15:29; Tit. 1:2; Ebr. 6:18; Eno. 1:6). Mtu adanganyaye na hatubu atatupwa nje, M&M 42:21. Waongo watarithi utukufu wa telestia, M&M 76:81, 103–106. Tunaamini katika kuwa waaminifu, M ya I 1:13.