Misaada ya Kujifunza
Elisha


Elisha

Nabii wa Agano la Kale wa ufalme wa Kaskazini wa Israeli na mshauri wa kuaminika wa wafalme kadhaa wa nchi hiyo.

Elisha alikuwa na tabia ya upole na mwenye moyo wa kupenda, pasipo ari ya moto mkali ambayo bwana wake, Eliya, walitofautiana. Miujiza yake yenye kutambulika (2 Fal. 2–5; 8) inashuhudia kwamba hakika alipokea nguvu za Eliya wakati yeye alipomrithi Eliya kama nabii (2 Fal. 2:9–12). Kwa mfano, aliyaponya maji ya chemchemi ya maji machungu, aliyagawanya maji ya Mto Yordani, alizidisha mafuta ya mjane, alimfufua mvulana kutoka kwa wafu, alimponya mtu wa ukoma, alisababisha shoka la chuma kuelea majini, na akawapiga Washuri kwa upofu (2 Fal. 2–6). Huduma yake ilidumu kwa zaidi ya miaka hamsini wakati wa utawala wa Yehoramu, Yehu, Yohoahazi, na Yoashi.