Msaada wa Masomo
Mpinga Kristo
iliyopita inayofuata

Mpinga Kristo

Mtu yoyote au kitu chochote ambacho kinaiga mpango wa injili ya kweli ya wokovu na kwamba kwa wazi au kwa siri kinampinga Kristo. Yohana Mfunuzi anamwelezea mpinga Kristo kama mdanganyifu (1 Yoh. 2:18–22; 4:3–6; 2 Yoh. 1:7). Mpinga Kristo mkuu ni Lusiferi, lakini anao wasaidizi wengi, viumbe wa kiroho na wa kimwili.