Misaada ya Kujifunza
Israeli


Israeli

Bwana alimpa Yakobo jina la Israeli, mwana wa Isaka na mjukuu wa Ibrahimu katika Agano la Kale (Mwa. 32:28; 35:10). Jina Israeli laweza kutumiwa kwa Yakobo mwenyewe, wazao wake, au kwa ufalme ambao wazao wake wakati fulani waliumiliki katika nyakati za Agano la Kale (2 Sam. 1:24; 23:3). Baada ya Musa kuwaongoza wana wa Israeli kutoka katika utumwa wa Misri (Ku. 3–14), walitawaliwa na waamuzi kwa zaidi ya miaka mia tatu. Wakianza na Mfalme Sauli, wafalme waliutawala muungano wa Israeli hadi kifo cha Sulemani, wakati makabila kumi yalipoasi kutoka kwa Rehoboamu ili kuanzisha taifa jingine. Baada ya ufalme wa Israeli kuwa umegawanyika, makabila ya kaskazini, kama sehemu iliyokuwa kubwa zaidi, yalishikilia jina la Israeli, wakati ule ufalme wa kusini ukaitwa Yuda. Nchi ya Kanaani pia siku hizi inaitwa Israeli. Katika maana nyingine, Israeli maana yake muumuni wa kweli wa Kristo (Rum. 10:1; 11:7; Gal. 6:16; Efe. 2:12).

Makabila kumi na mawili ya Israeli

Mjukuu wa Ibrahimu, Yakobo, ambaye jina lake lilibadilishwa na kuwa Israeli, alikuwa na wana kumi na wawili. Wazao wao wamekuja kujulikana kama makabila kumi na mawili ya Israeli au wana wa Israeli. Haya ndiyo makabila hayo kumi na mawili: Reubeni, Simeoni, Lawi, Yuda, Isakari, na Zebuluni (wana wa Yakobo na Lea); Dani, na Naftari (wana wa Yakobo na Bilha); Gadi na Asheri (wana wa Yakobo na Zilpa); Yusufu na Benjamini (wana wa Yakobo na Raheli) (Mwa. 29:32–30:24; 35:16–18).

Yakobo alimpa kila kiongozi wa kikabila baraka kabla ya kifo chake (Mwa. 49:1–28). Kwa taarifa zaidi, ona jina la kila mwana wa Yakobo.

Reubeni, mwana wa kiume wa kwanza wa mke wa kwanza wa Yakobo, Lea, alipoteza baraka ya haki yake ya uzaliwa wa kwanza na sehemu mbili ya urithi kwa sababu ya ukosefu wa maadili (Mwa. 49:3–4). Haki hiyo ya uzaliwa wa kwanza hatimaye ilikwenda kwa Yusufu, ambaye alikuwa mwana wa kwanza wa mke wa pili wa Yakobo, Raheli (1 Nya. 5:1–2). Lawi, ambaye kabila lake Bwana alikuwa amelichagua kumtumikia kama makuhani walio wahudumu Wake, hakupokea urithi kwa sababu ya wito wao maalumu wa kuhudumu miongoni mwa makabila yote. Hii iliruhusu sehemu mbili zigawiwe kwa wana wa Yusufu, Efraimu na Manase (1 Nya. 5:1; Yer. 31:9), ambao walihesabiwa kama makabila tofauti ya Israeli (TJS, Mwa. 48:5–6).

Watu wa kabila la Yuda walitakiwa kuwa watawala hadi Masiya alipokuja (Mwa. 49:10; TJS Mwa. 50:24 [Kiambatisho]). Katika siku za mwisho, kabila la Efraimu litakuwa na nafasi ya kupeleka ujumbe wa Urejesho wa injili ulimwenguni na kuwakusanya Israeli waliotawanyika (Kum. 33:13–17). Wakati utafika ambao kupitia injili ya Yesu Kristo, Efraimu atakuwa katika nafasi ya uongozi katika kuyaunganisha makabila yote ya Israeli (Isa. 11:12–13; M&M 133:26–34).

Kutawanyika kwa Israeli

Bwana aliwatawanya na kuwatesa makabila kumi na mawili ya Israeli kwa sababu ya uovu na uasi wao. Hata hivyo, Bwana pia alitumia kutawanyika huku kwa watu wateule Wake miongoni mwa mataifa ya ulimwengu ili kuyabariki mataifa hayo.

Kukusanyika kwa Israeli

Nyumba ya Israeli itakusanywa pamoja katika siku za mwisho kabla ya ujio wa Kristo (M ya I 1:10). Bwana huwakusanya watu Wake Israeli wanapomkubali Yeye na kuzishika amri Zake.

Makabila Kumi ya Israeli yaliyopotea

Makabila haya kumi ya Israeli yaliunda ufalme wa kaskazini wa Israeli na walichukuliwa mateka katika Ashuru mwaka 721 K.K. Wakati huo walikwenda katika “nchi za kaskazini” na wakawa wamepotea katika ufahamu wa wenzao. Katika siku za mwisho watarudi.