Misaada ya Kujifunza
Nasaba


Nasaba

Kumbukumbu iliyoandikwa kufuatia mstari wa uzao katika familia. Ambapo ofisi za ukuhani au baraka fulani zilizuiliwa kwa familia fulani tu, nasaba katika maandiko zilikuwa muhimu sana (Mwa. 5; 10; 25; 46; 1 Nya. 1–9; Ezra 2:61–62; Neh. 7:63–64; Mt. 1:1–17; Lk. 3:23–38; 1 Ne. 3:1–4; 5:14–19; Yar. 1:1–2). Katika Kanisa lililorejeshwa siku hizi, waumini wa Kanisa wanaendelea kufuatilia mstari wa uzao wa familia zao, kwa upande mmoja ili kuwatambua kiusahihi walengwa wao waliofariki ili waweze kufanya ibada za wokovu kwa niaba ya walengwa wao. Ibada hizi zipo kwa ajili ya watu wale waliofariki ambao wanaikubali injili ya Yesu Kristo katika ulimwengu wa roho (M&M 127–128).