Misaada ya Kujifunza
Malimbuko


Malimbuko

Mavuno ya kwanza yaliyokusanywa katika msimu. Katika nyakati za Agano la Kale, yalitolewa kwa Bwana (Law. 23:9–20). Yesu Kristo alikua limbuko kwa Mungu katika hilo, kwamba Yeye alikuwa wa kwanza kufufuliwa (1 Kor. 15:20, 23; 2 Ne. 2:9). Wale ambao wanaipokea injili na kustahimili hadi mwisho katika uaminifu ni njia ya ishara ya malimbuko, kwani wao ni mali ya Mungu.