Misaada ya Kujifunza
Yona


Yona

Nabii wa Agano la Kale aliyeitwa na Bwana kuhubiri toba katika mji wa Ninawi (Yon. 1:1–2).

Kitabu cha Yona

Kitabu katika Agano la Kale ambacho kinaelezea juu ya tukio moja katika maisha ya Yona. Yona yawezekana hakuandika kitabu hiki yeye mwenyewe. Wazo kuu la kitabu cha Yona ni kwamba Yehova anatawala kila mahali na upendo Wake hauzuiliwi katika taifa moja au watu fulani tu.

Katika mlango wa 1, Bwana anamwita Yona kwenda kuhubiri Ninawi. Badala ya kufanya kama Bwana alivyomwamuru, Yona alitoroka kwa mashua na akamezwa na samaki mkubwa. Katika Mlango wa 2, Yona alisali kwa Bwana, na yule samaki akamtapika Yona nje kwenye ardhi kavu. Mlango wa 3 unaandikwa kuwa Yona alikwenda Ninawi na akatoa unabii wa kuanguka kwa mji huo. Hata hivyo, watu wale wakatubu. Katika Mlango wa 4, Bwana anamkanya Yona kwa kukasirika kwa vile Bwana aliwaokoa wale watu.

Yesu alifundisha kwamba Yona kumezwa na samaki kumetumika kama ishara ya mauti ya Yesu mwenyewe na ufufuko wake (Mt. 12:39–40; 16:4; Lk. 11:29–30).