Misaada ya Kujifunza
Enoshi, Mwana wa Yakobo


Enoshi, Mwana wa Yakobo

Nabii Mnefi na mtunza kumbukumbu katika Kitabu cha Mormoni ambaye alisali na kupata msamaha wa dhambi zake kwa njia ya imani yake katika Kristo (Eno. 1:1–8). Bwana aliagana na Enoshi kukitoa Kitabu cha Mormoni kwa Walamani (Eno. 1:15–17).

Kitabu cha Enoshi

Ni kitabu katika Kitabu cha Mormoni ambacho huzungumzia juu ya sala ya Enoshi kwa Bwana kwa ajili ya msamaha wa kibinafsi, kwa ajili ya watu wake, na kwa ajili ya wengine. Bwana akamwahidi kwamba Kitabu cha Mormoni kingehifadhiwa na kitolewe kwa Walamani katika siku zijazo. Ingawa kitabu hicho kuna mlango moja pekee, kinaandika hadithi yenye nguvu ya mtu ambaye alimtafuta Mungu wake katika sala, aliishi kwa kutii amri za Mungu, na kabla ya kifo chake alifurahia katika kumjua kwake Mkombozi.