Misaada ya Kujifunza
Nauvoo, Illinois (Marekani)


Nauvoo, Illinois (Marekani)

Mji ulioanzishwa na Watakatifu wa siku za Mwisho katika mwaka 1839 katika jimbo la Illinois. Uko kando ya Mto Mississippi, karibu maili 200 (kilomita 320) juu ya mto kutoka St. Louis.

Kutokana na mateso katika jimbo la Missouri, Watakatifu walihamia karibu maili 200 (kilometa 320) kaskazini mashariki, ngʼambo ya Mto Mississippi, na ndani ya Illinois, mahali ambapo walipata hali iliyowavutia zaidi. Hatimaye, Watakatifu walinunua ardhi karibu na mji ambao haukuendelea wa Commerce. Nchi hii kwa kweli ilikuwa msitu uliojaa maji pamoja na majengo machache ya kawaida. Watakatifu waliyakausha maji katika ardhi na wakajenga majumba. Joseph Smith aliihamishia familia yake katika nyumba ndogo ya mbao. Jina la Commerce la mji huo likabadilishwa kuwa Nauvoo, kwa neno la Kiebrania maana yake “mrembo.”

Sehemu kadhaa za Mafundisho na Maagano ziliandikwa Nauvoo (M&M 124–129; 132; 135). Watakatifu waliambiwa kujenga hekalu katika Nauvoo (M&M 124:26–27). Walijenga hekalu na kuunda vigingi vya Sayuni kabla ya kufukuzwa kutoka majumbani mwao katika mwaka 1846. Kama matokeo ya mateso haya, Watakatifu waliondoka katika eneo na kufanya safari yao kwenda magharibi.