Misaada ya Kujifunza
Nathani


Nathani

Nabii wa Agano la Kale katika wakati wa Mfalme Daudi. Daudi alipojitolea kujenga hekalu la Bwana, Bwana alimwelekeza Nathani kumwambia Daudi asijenge. Nathani pia alimkemea Daudi kwa kusababisha mauti ya Uria, mmoja wa askari wake, na kwa kumchukua mke wa Uria, Bathsheba (2 Sam. 12:1–15; M&M 132:38–39). Sadoki, pamoja na Nathani, walimpaka mafuta mfalme Sulemani mwana wa Daudi (1 Fal. 1:38–39, 45).