Jina lenye hadhi na ni heshima kubwa kwa Mungu Baba na Mwokozi Yesu Kristo. Jina hili linaonyesha nafasi Zao kama watawala wakuu na wenye upendo wa viumbe Vyao.
Hakuna kitu kigumu zaidi kwa Bwana, Mwa. 18:14 .
Bwana alisema na Musa uso kwa uso, Ku. 33:11 .
Mpende Bwana Mungu wako, Kum. 6:5 (Mt. 22:37 ; Mk. 12:30 ).
Lakini mimi na nyumba yangu, tutamtumikia Bwana, Yos. 24:15 .
Bwana ndiye mchungaji wangu, Zab. 23:1 .
Bwana ni hodari na mwenye uwezo, uwezo wa vita, Zab. 24:8 .
Bwana Yehova ndiye nguvu yangu, Isa. 12:2 (2Â Ne. 22:2 ).
Mimi, Bwana ni Mwokozi wako na Mkombozi wako, Isa. 60:16 .
Utamwabudu Bwana Mungu wako, Mt. 4:10 (Lk. 4:8 ).
Ni makuu jinsi gani makuu aliyotutendea Bwana, Mk. 5:19 .
Kuna Bwana mmoja Yesu Kristo, 1Â Kor. 8:6 .
Kuna Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja, Efe. 4:5 .
Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni, 1Â The. 4:16 .
Nitakwenda na kufanya mambo yale Bwana ameyoniamuru, 1Â Ne. 3:7 .
Bwana atawahukumu maskini kwa haki, 2Â Ne. 30:9 .
Bwana Mungu, Mungu wa Ibrahimu, aliwakomboa Waisraeli kutoka utumwani, Alma 29:11 .
Hakuna kinachoweza kuwaokoa watu isipokuwa toba na imani juu ya Bwana, Hel. 13:6 (Mos. 3:12 ).
Sikiliza maneno ya Yesu Kristo, Bwana wako, M&M 15:1 .
Utafuteni uso wa Bwana daima, M&M 101:38 .
Bwana atakuwa mwekundu katika mavazi yake wakati wa Ujio wa Pili, M&M 133:48 (Isa. 63:1–4 ).
Ibrahimu aliongea na Bwana uso kwa uso, Ibr. 3:11 .
Tunaamini kuwa kanuni ya kwanza ya injili ni imani katika Bwana Yesu Kristo, M ya I 1:4 .