Msaada wa Masomo
Toa unabii, Unabii
iliyopita inayofuata

Toa unabii, Unabii

Unabii una maneno matakatifu ya kimungu au maandishi, ambayo mtu hupokea kwa njia ya ufunuo kutoka kwa Roho Mtakatifu. Ushuhuda wa Yesu ni roho ya unabii (Ufu. 19:10). Unabii waweza kuwa juu ya mambo yaliyopita, yaliyopo, au yajayo. Mtu anapotoa unabii, hunena au huandika lile ambalo Mungu anataka yeye alijue, kwa manufaa yake mwenyewe au kwa manufaa ya wengine. Watu binafsi wanaweza kupokea unabii au ufunuo kwa ajili ya maisha yao wao wenyewe.