Msaada wa Masomo
Komboa, Kombolewa, Ukombozi
iliyopita inayofuata

Komboa, Kombolewa, Ukombozi

Kuokoa, kununua, au kufidia, kama vile kumweka mtu huru kutokana na utumwa kwa kufanya malipo. Ukombozi unahusu Upatanisho wa Yesu Kristo na kuokolewa kutoka katika dhambi. Upatanisho wa Yesu huwakomboa wanadamu wote kutoka katika mauti ya kimwili. Kupitia Upatanisho Wake, watu walio na imani katika Yeye na wenye kutubu pia hukombolewa kutoka katika mauti ya kiroho.