Misaada ya Kujifunza
Wakorintho, Waraka kwa


Wakorintho, Waraka kwa

Vitabu viwili vilivyoko katika Agano Jipya. Mwanzoni zilikuwa ni barua ambazo Paulo aliwaandikia Watakatifu katika Korintho ili kusahihisha mvurugano miongoni mwao. Wakorintho waliishi katika jumuiya ambayo ilikuwa ovu kimaadili.

Wakorintho wa Kwanza

Mlango wa 1 una salamu za Paulo na maonyo yake madogo kwa watakatifu kuungana Mlango wa 2–6 ni masahihisho ya Paulo juu ya makosa ya Watakatifu wa Korintho. Mlango wa 7–12 ni majibu ya Paulo ya maulizo aliyoulizwa. Mlango wa 13–15 ni mambo yahusuyo hisani, vipawa vya kiroho, na Ufufuko. Mlango wa 16 una maonyo ya Paulo juu ya kusimama imara katika imani.

Wakorintho wa Pili

Mlango wa 1 una salamu za Paulo na ujumbe wa kufariji. Mlango wa 2 una ushauri binafsi kwa Tito. Mlango wa 3–7 inahusu uwezo wa injili katika maisha ya Watakatifu na viongozi wao. Mlango wa 8–9 inawaasa Watakatifu kuwa watoaji wenye moyo wa furaha kwa maskini. Mlango wa 10–12 ni maelekezo ya Paulo mwenye nafasi yake kama Mtume. Mlango wa 13 ni maonyo ya kuwa wakamilifu.