Misaada ya Kujifunza
Wana wa Upotevu


Wana wa Upotevu

Wafuasi wa Shetani watakaoteseka pamoja naye milele. Wana wa upotevu ni pamoja na (1) wale waliomfuata Shetani na wakafukuzwa kutoka mbinguni kwa ajili ya uasi katika maisha kabla ya kuwa duniani na (2) wale walioruhusiwa kuzaliwa katika ulimwengu huu wakiwa na miili lakini halafu wakamtumikia Shetani na wakamgeuka kabisa Mungu. Wale walio katika kundi hili la pili watafufuka kutoka kwa wafu lakini hawatakombolewa kutokana na mauti ya pili (kiroho) na hawataweza kukaa katika ufalme wa utukufu (M&M 88:32, 35).