Misaada ya Kujifunza
Wafalme


Wafalme

Vitabu viwili katika Agano la Kale. Vitabu hivi vinasimulia historia ya Israeli kuanzia uasi wa Adoniya, mwana wa nne wa mfalme Daudi (karibu mwaka 1015 K.K.), hadi utumwa wa mwisho wa Yuda (karibu mwaka 586 K.K.). Ni pamoja na historia nzima ya ufalme wa kaskazini (makabila kumi ya Israeli) tangu kutengana kwao hadi Waashuru walipowachukua mateka katika nchi za kaskazini. Ona pia Wendo katika kiambatisho.

Wafalme wa Kwanza

Mlango wa 1 unaelezea siku za mwisho za maisha ya Mfalme Daudi. Mlango wa 2–11 ni juu ya maisha ya Sulemani. Mlango wa 12–16 inazungumzia juu ya warithi wa karibu wa Sulemani, Rehoboamu na Yeroboamu. Yeroboamu alisababisha mgawanyiko wa ufalme wa Israeli. Wafalme wengine pia wametajwa. Mlango wa 17–21 inaelezea sehemu ya huduma ya Eliya kama alivyomwonya Ahabu, mfame wa Israeli. Mlango wa 22 ni juu ya vita dhidi ya Shamu ambayo Ahabu na Yehoshafati, mfalme wa Yuda, alishiriki. Nabii Mika alitoa unabii dhidi ya wafalme hawa.

Wafalme wa Pili

Mlango 1:1–2:11 inaendeleza juu ya maisha ya Eliya, ikiwa pamoja na Eliya kutwaliwa mbinguni katika gari ya kukokotwa na farasi wa moto. Mlango 2–9 ni juu ya huduma ya Eliya ya imani na uwezo mkuu. Mlango 10 unaelezea juu ya Yehu, mfalme, na namna alivyoiangamiza nyumba ya Ahabu na makuhani wa Baali. Mlango 1–13 ni juu ya utawala wa haki ya Yehoashi na kifo cha Elisha. Mlango 14–17 inaeleza juu ya wafalme mbalimbali waliotawala katika Israeli na Yuda, mara kwa mara katika uovu. Mlango 15 unaandikwa juu ya Waashuru kuyateka makabila kumi ya Israeli. Mlango 18–20 inaandikwa juu ya maisha ya haki ya Hezekia, mfalme wa Yuda, na nabii Isaya. Mlango 21–23 inasimulia juu ya wafalme Manase na Yosia. Kulingana na mapokeo, Manase ndiye anayewajibika kwa mauaji ya mfiadini ya Isaya. Yosia alikuwa mfalme mwaminifu aliyeianzisha tena sheria miongoni mwa Wayahudi. Mlango 24–25 inaandika juu ya utumwa katika Babeli.