Misaada ya Kujifunza
Imanueli


Imanueli

Mojawapo ya majina ya Yesu Kristo. Linatokana na maneno ya Kiebrania ambayo maana yake “Mungu pamoja nasi.”

Imanueli ni jina na cheo kilichotolewa kama ishara ya kukombolewa na Mungu (Isa. 7:14). Maneno ya Isaya kwa Imanueli yametambuliwa hususani na Mathayo kama unabii juu ya kuzaliwa kwa Yesu katika mwili wa kufa (Mt. 1:18–25). Jina hili pia linaonekana katika maandiko ya siku za mwisho (2 Ne. 17:14; 18:8; M&M 128:22).