Misaada ya Kujifunza
Gadi, Mwana wa Yakobo


Gadi, Mwana wa Yakobo

Katika Agano la Kale, ni mwana wa Yakobo na Zilpa (Mwa. 30:10–11). Wazao wake wakawa kabila la Israeli.

Kabila la Gadi

Kwa ajili ya baraka za Yakobo juu ya mwanawe Gadi, ona Mwanzo 49:19. Kwa ajili ya baraka za Musa juu ya kabila la Gadi, ona Kumbukumbu la Torati 33:20–21. Kulingana na baraka hizi, wazao wa Gadi walikuwa wawe watu wa vita. Ardhi iliyogawiwa kwao katika nchi ya Kanaani ilikuwa mashariki ya Mto Yordani nayo ilikuwa nchi ya malisho mazuri na yenye maji mengi.