Misaada ya Kujifunza
Alma, Mwana wa Alma


Alma, Mwana wa Alma

Katika Kitabu cha Mormoni, ni mwamuzi mkuu wa kwanza na nabii katika taifa la Wanefi. Katika miaka yake ya mwanzoni yeye alitafuta kuliangamiza Kanisa (Mos. 27:8–10). Hata hivyo malaika akamtokea naye akaongolewa katika injili (Mos. 27:8–24; Alma 36:6–27). Baadaye aliiacha nafasi yake kama mwamuzi mkuu ili kuwafundisha watu (Alma 4:11–20).

Kitabu cha Alma

Kitabu kimojawapo katika Kitabu cha Mormoni, kina ufupisho wa kumbukumbu ya nabii Alma, mwana wa Alma, na mwanawe Helamani. Matukio yaliyoelezwa katika kitabu hicho yalitokea Karibia mwaka 91 hadi 52 kabla ya Kristo. Kitabu hiki kina milango 63. Mlango wa 1–4 inaelezea uasi wa wafuasi wa Nehori na Amlisi dhidi ya Wanefi. Vita vilivyotokea kama matokeo yake vilikuwa miongoni mwa vita vilivyoleta uharibifu mkubwa katika historia ya Wanefi. Mlango wa 5–16 ina historia ya safari za awali za kimisionari za Alma, ikiwa ni pamoja na mahubiri yake juu ya Mchungaji Mwema (Alma 5) na kuhubiri kwake akiwa pamoja na Amuleki katika mji wa Amoniha. Mlango wa 17–27 ina kumbukumbu ya wana wa Mosia na huduma yao miongoni mwa Walamani. Mlango wa 28–44 ina baadhi ya mahubiri muhimu zaidi ya Alma. Katika mlango wa 32 Alma analinganisha neno na mbegu; katika mlango wa 36 anasimulia mwanawe Helamani hadithi ya kuongolewa kwake. Mlango wa 39–42 anaandika maonyo ya Alma kwa mwanawe Koriantoni, ambaye amekuja kujihusisha na uzinzi; mahubiri haya muhimu yanaelezea juu ya haki, huruma, Ufufuko, na Upatanisho. Mlango wa 45–63 inaelezea vita vya Wanefi vya kipindi hicho na uhamiaji chini ya Hagothi. Viongozi maarufu kama vile Kapteni Moroni, Teankumu, na Lehi walisaidia katika kuwalinda Wanefi kwa njia ya ujasiri wao na matendo yao katika wakati uliofaa.