Misaada ya Kujifunza
Amosi


Amosi

Nabii wa Agano la Kale aliyetoa unabii karibia mwaka 792 hadi 740 K.K. Katika siku za Uzia, mfalme wa Yuda, na Yeroboamu, mfalme wa Israeli.

Kitabu cha Amosi

Ni kitabu katika Agano la Kale. Unabii mwingi wa Amosi unawaonya Waisraeli na mataifa ya jirani yake kuigeukia haki.

Mlango wa 1–5 inaiita Israeli na mataifa ya jirani yake kwenye toba. Mlango wa 3 unaeleza kwamba Bwana huwafunulia siri Zake manabii na kwamba kwa sababu ya dhambi, Israeli ataangamizwa na adui. Mlango wa 6–8 inatoa unabii juu ya anguko la Israeli miaka mingi kabla ya uvamizi wa Waashuru. Mlango wa 9 unatoa unabii kwamba Israeli watarejeshwa katika nchi yao yenyewe.