Misaada ya Kujifunza
Koreshi


Koreshi

Katika Agano la Kale, ni mfalme wa Uajemi ambaye aliutimiza unabii wa Isaya (2 Nya. 36:22–23; Isa. 44:28; 45:1) kwa kuwaruhusu Wayahudi kurudi Yerusalemu ili kulijenga tena hekalu, na hivyo alipendelea kumalizika kwa utumwa wa Babilonia. Unabii wa Isaya ulifanyika kiasi cha miaka 180 kabla ya tendo hili la mfalme.