Misaada ya Kujifunza
Danieli


Danieli

Mhusika mkuu wa kitabu cha Danieli katika Agano la Kale; ni nabii wa Mungu na ni mtu aliyekuwa na imani kubwa.

Hakuna kitu kinachojulikana juu ya wazazi wake, ingawa anaonekana kuwa ametokana na uzao wa kifalme (Dan. 1:3). Alichukuliwa mateka kwenda Babeli, mahali ambako alipata jina la Belteshaza (Dan. 1:6–7). Danieli na mateka wengine watatu walikataa chakula cha mfalme kwa sababu za kidini (Dan. 1:8–16).

Danieli alipata kukubalika na Nebukadneza na Dario kutokana na uwezo wake wa kutafsiri ndoto (Dan. 2; 4; 6). Pia alisoma na kutafsiri maandiko ya mkono yaliyoandikwa ukutani (Dan. 5). Maadui zake walikula njama dhidi yake, naye akatupwa katika tundu la simba, lakini Bwana akayalinda maisha yake (Dan. 6).

Kitabu cha Danieli

Kitabu hiki kina sehemu mbili: mlango wa 1–6 ni hadithi juu ya Danieli na wenzake watatu; mlango wa 7–12 ni maono ya kinabii ambayo Danieli aliyaona. Kitabu hiki kinafundisha umuhimu wa kuwa wa kweli kwa Mungu na kinaelezea kwamba Bwana huwabariki walio waaminifu.

Mchango mkubwa wa kitabu hiki ni tafsiri ya ndoto ya Mfalme Nebukadneza. Katika ndoto hiyo, ufalme wa Mungu katika siku za mwisho unasimama kama jiwe ambalo limekatwa kutoka mlimani. Jiwe hilo litabiringika hadi liijaze dunia yote (Dan. 2; ona pia M&M 65:2).