Misaada ya Kujifunza
Neema


Neema

Nguvu yenye kuwezesha itokayo kwa Mungu ambayo huwaruhusu wanaume na wanawake kupata baraka katika maisha haya na kupata uzima wa milele na kuinuliwa baada ya kuonyesha imani, kutubu, na kufanya jitihada zao zilizo bora ili kushika amri. Msaada mtakatifu wa aina hii au nguvu hii hutolewa kwa njia ya rehema na upendo wa Mungu. Kila mtu mwenye mwili ufao anahitaji neema takatifu kwa sababu ya Anguko la Adamu na pia kwa sababu ya udhaifu wa mwanadamu.