Misaada ya Kujifunza
Waebrania, Waraka kwa


Waebrania, Waraka kwa

Kitabu katika Agano Jipya. Paulo aliandika barua hii kwa waumini wa Kanisa wa Kiyahudi ili kuwahimiza kwamba sehemu muhimu za sheria ya Musa zimetimia katika Kristo na kwamba sheria ya juu kabisa ya injili imekuja badala yake. Paulo aliporudi Yerusalemu mwishoni mwa safari yake ya tatu ya kuhubiri (karibu mwaka 60 B.K.), alikuta kwamba waumini wa Kanisa wa Kiyahudi wengi walikuwa bado wakiishi kwa sheria ya Musa (Mdo. 21:20). Hii ilikuwa karibu miaka kumi baada ya mkutano wa Kanisa huko Yerusalemu uliokuwa umeazimia kwamba baadhi ya ibada za sheria ya Musa hazikuwa muhimu kwa wokovu wa Wakristo wayunani. Ni dhahiri, mara baada ya hapo, Paulo aliwaandikia Waebrania ili kuwaonyesha andiko lao wenyewe na kwa nguvu ya hoja ya kwa nini wao hawapaswi tena kutenda sheria ya Musa.

Mlango wa 1 na 2 inaeleza kwamba Yesu ni mkuu kuliko malaika. Mlango wa 3–7 inamlinganisha Yesu na Musa na kwa sheria ya Musa na inashuhudia kwamba Yeye ni mkuu kuliko wote. Pia hufundisha kwamba Ukuhani wa Melkizedeki ni mkuu kuliko wa Haruni. Mlango wa 8–9 inaelezea namna ibada za sheria za Musa zilivyokuwa zikiwaandaa watu kwa ajili ya huduma ya Kristo na namna Kristo alivyo mpatanishi wa agano jipya (Alma 37:38–45; M&M 84:21–24). Mlango wa 10 unahimiza bidii na uaminifu. Mlango wa 11 ni mafundisho juu ya imani. Mlango wa 12 unatoa maonyo na salamu. Mlango wa 13 unafundisha juu ya tabia ya kuheshimiwa kwa ndoa na umuhimu wa utiifu.