Misaada ya Kujifunza
Uzinzi


Uzinzi

Ushirikiano wa kingono usio wa kisheria kati ya wanaume na wanawake. Ingawa uzinzi kwa ujumla huelezea tendo la ngono kati ya mtu aliyeoa au kuolewa na mtu mwingine asiye mme au mke wake, katika maandiko pia yaweza kumaanisha kwa wasiooa au kuolewa.

Nyakati zingine uzinzi unatumika kama ishara ya uasi wa taifa au watu wote kutoka katika njia za Bwana (Hes. 25:1–3; Yer. 3:6–10; Eze. 16:15–59; Hos. 4).