Misaada ya Kujifunza
Baali


Baali

Ni mungu-jua mwanamume aliyekuwa akiabudiwa kwa kawaida katika Fonisia (1 Fal. 16:31) lakini pia aliabudiwa katika njia tofauti katika sehemu mbali mbali na Wamoabii kama Baali-Peori (Hes. 25:1–3), huko Shekemu kama Baali-bethiri (Amu. 8:33; 9:4), huko Ekroni kama Baali-Zebubu (2 Fal. 1:2). Baali aweza kuwa huyo huyo Beli wa Babilonia na Zayo wa Uyunani. Neno Baali linaelezea uhusiano kati ya bwana na mtumwa wake. Alama ya kawaida ya Baali ilikuwa ngʼombe dume. Ashtorethi alikuwa mungu mwanamke ambaye kwa kawaida aliabudiwa pamoja na Baali.

Baali nyakati zingine liliunganishwa na jina jingine au neno ili kuonyesha uhusiano na Baali, kama vile mahali alipokuwa akiabudiwa, au mtu aliyefikiriwa kuwa na tabia kama za Baali. Baadaye, kwa sababu Baali lilikuja kuwa na maana ovu sana, neno Boshethi lilichukua mahali pake katika majina yale yaliyounganishwa nayo. Boshethi maana yake “aibu.”