Mwanzoni mwa Enzi ya Milenia, Kristo atarudi duniani. Tukio hili litaonyesha ule mwisho wa kipindi cha majaribu cha mwili wenye kufa cha dunia hii. Waovu wataondolewa kutoka duniani na waadilifu watatwaliwa katika wingu wakati dunia ikisafishwa. Wakati hakuna mwanadamu ajuaye hasa lini Kristo atakuja kwa mara ya pili, Yeye ametupa sisi ishara za kuzitazamia ambazo zinaashiria wakati umekaribia (Mt. 24 ; JS—M 1 ).
Ninajua kwamba Mkombozi wangu katika siku ya mwisho atasimama juu ya dunia, Ayu. 19:25 .
Mbele zangu kila goti litapigwa, kila ulimi utaapa, Isa. 45:23 (M&M 88:104 ).
Mwana wa Mtu alikuja kwa mawingu ya mbinguni, Dan. 7:13 (Mt. 26:64 ; Lk. 21:25–28 ).
Watanitazama mimi ambaye walimchoma, Zek. 12:10 .
Mtu atasema, Je, jeraha hizi mikononi mwako ni nini, Zek. 13:6 (M&M 45:51 ).
Ni nani atakayestahmili hadi katika siku ya kuja kwake? kwa maana yeye ni kama moto wa mtu asafishaye fedha, Mal. 3:2 (3Â Ne. 24:2 ; M&M 128:24 ).
Mwana wa Mtu atakuja katika utukufu wa Baba yake, Mt. 16:27 (Mt. 25:31 ).
Juu ya siku ile na saa ile hakuna mtu ajuaye, ila Baba yangu peke yake, Mt. 24:36 (M&M 49:7 ; JS—M 1:38–48 ).
Huyu Yesu atakuja jinsi hiyo hiyo mlivyomwona akienda zake mbinguni, Mdo. 1:11 .
Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni, 1Â The. 4:16 .
Siku ya Bwana itakuja kama mwivi ajavyo usiku, 2Â Pet. 3:10 .
Bwana atakuja pamoja na maelfu kumi ya Watakatifu wake, Yuda 1:14 .
Yuaja na mawingu, na kila jicho litamwona, Ufu. 1:7 .
Jitayarisheni, jitayarisheni, kwa maana Bwana yu karibu, M&M 1:12 .
Nitajifunua mwenyewe kutoka mbinguni kwa uwezo, na kukaa duniani miaka elfu, M&M 29:9–12 .
Pazeni sauti zenu na kutangaza toba, mkimtengenezea Bwana njia kwa ujio wake wa pili, M&M 34:5–12 .
Mimi ndimi Yesu Kristo, nami nitakuja ghafla hekaluni mwangu, M&M 36:8 (M&M 133:2 ).
Siku i karibu kuja ambayo mtaniona, na kujua kuwa Mimi ndimi, M&M 38:8 .
Yule aniogopaye mimi atazitazamia ishara za kuja kwa Mwana wa Mtu, M&M 45:39 .
Uso wa Bwana utafunuliwa, M&M 88:95 .
Siku ile iliyo kuu na ya kutisha ya Bwana i karibu, M&M 110:16 .
Wakati Mwokozi atakapoonekana tutamwona yeye kama alivyo, M&M 130:1 .
Mwokozi atasimama katikati ya watu wake na atatawala, M&M 133:25 .
Huyu ni nani ashukaye kutoka kwa Mungu mbinguni akiwa na mavazi yaliyotiwa rangi, M&M 133:46 (Isa. 63:1 ).