Misaada ya Kujifunza
Ono


Ono

Ufunuo wa kuona juu ya tukio fulani, mtu, au jambo kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.

Mifano ya maono muhimu ni pamoja na yafuatayo: Ono la Ezekieli juu ya siku za mwisho (Eze. 37–39), ono la Stefano juu ya Yesu kusimama mkono wa kuume wa Mungu (Mdo. 7:55–56), ufunuo wa Yohana kuhusu siku za mwisho (Ufu. 4–21), ono la Lehi na Nefi juu ya mti wa uzima (1 Ne. 8; 10–14), ono la Alma Mtoto juu ya malaika wa Bwana (Mos. 27), ono la kaka wa Yaredi juu ya wakazi wote wa dunia (Eth. 3:25), ono la madaraja ya utukufu (M&M 76), maono waliyopewa Joseph Smith na Oliver Cowdery katika hekalu la Kirtland (M&M 110), ono la Joseph F. Smith juu ya ukombozi wa wafu (M&M 138), ono la Musa juu ya Mungu na uumbaji Wake (Musa 1), ono la Enoshi juu ya Mungu (Musa 6–7), na Ono la Kwanza la Joseph Smith (JS—H 1).