Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 76


Sehemu ya 76

Ono lililotolewa kwa Joseph Smith Nabii na Sidney Rigdon, huko Hiram, Ohio, 16 Februari 1832. Katika utangulizi wa kumbukumbu ya ono hili, Historia ya Joseph Smith inaeleza: “Baada ya kurejea kutoka kwenye mkutano huko Amherst, nilianza tena tafsiri ya Maandiko. Kutokana na mafunuo mbali mbali ambayo nilikuwa nimekwisha yapokea, ilionekana dhahiri kwamba vipengele vingi muhimu vinavyogusa wokovu wa mwanadamu, vilikuwa vimeondolewa kutoka kwenye Biblia, au vilipotezwa kabla haijatungwa. Ilionekana wazi kutokana na ukweli uliosalia, kwamba kama Mungu alimzawadia kila mtu kulingana na matendo aliyoyafanya katika mwili neno ‘Mbingu,’ kama linavyo kusudiwa na Watakatifu kuwa makao ya milele, ni lazima ziwe falme zaidi ya moja. Vivyo hivyo, … wakati nikitafsiri injili ya Mt. Yohana, mimi mwenyewe na Mzee Rigdon tuliona ono lifuatalo” Wakati ono hili likitolewa, Nabii alikuwa akitafsiri Yohana 5:29.

1–4, Bwana ndiye Mungu; 5–10, Siri za ufalme zitafunuliwa kwa wote walio waaminifu; 11–17, Wote watafufuka katika ufufuo wa wenye haki au wasio na haki; 18–24, Wakazi wa dunia nyingi ni wana au mabinti wa Mungu kwa njia ya Upatanisho wa Yesu Kristo; 25–29, Malaika wa Mungu alianguka na kuwa ibilisi; 30–49, Wana wa upotevu watateseka kwa dhambi ya milele; wengine wote watapata kiwango fulani cha wokovu; 50–70, Utukufu na tuzo za viumbe walioinuliwa katika ufalme wa selestia unaelezewa; 71–80, Wale watakao urithi ufalme terestria wanaelezwa; 81–113, Hali za wale walio katika fahari za telestia, terestria, na selestia zinafafanuliwa; 114–119, Wanaoamini wanaweza kuona na kuelewa siri za ufalme wa Mungu kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.

1 aSikieni, Enyi mbingu, na tega sikio, Ewe nchi, na shangilieni ninyi wakazi wake, kwa kuwa Bwana ndiye bMungu, na zaidi yake yeye chapana dMwokozi.

2 Hekima yake ni akuu, njia zake ni za bajabu, na hakuna awezaye kuona upana wa matendo yake.

3 aMakusudi yake hayashindwi, wala hakuna awezaye kuzuia mkono wake.

4 Tangu milele hata milele yeye ni ayule yule, na miaka yake bhaikomi.

5 Kwani hivyo ndivyo asemavyo Bwana—Mimi, Bwana, ni mwenye ahuruma na neema kwa wale wote bwanichao, na napenda kuwaheshimu wale wote ambao chunitumikia katika haki na kweli hata mwisho.

6 Tuzo lao litakuwa kuu na autukufu wao utakuwa wa milele.

7 Na kwao anitafunua bsiri zote, ndiyo, siri zote za ufalme zilizofichwa tangu siku za kale, na za zama zijazo, nitawafahamisha uradhi wa mapenzi yangu yanayohusu mambo yote ya ufalme wangu.

8 Ndiyo, hata maajabu ya milele watayajua, na mambo yajayo nitawaonyesha, hata mambo ya vizazi vingi.

9 Na ahekima yao itakuwa kuu, na bufahamu wao utafika mbinguni; na mbele zao akili za watu wenye akili czitapotea, na ufahamu wa wenye busara utafichwa.

10 Kwani kwa aRoho wangu bnitawaangaza, na kwa cuwezo wangu nitawajulisha siri za mapenzi yangu—ndiyo, hata mambo yale ambayo djicho halijayaona, wala sikio kusikia, wala hayajaingia katika moyo wa mwanadamu.

11 Sisi, Joseph Smith, Mdogo, na Sidney Rigdon, tukiwa akatika Roho tarehe kumi na sita ya Februari, katika mwaka wa Bwana wetu elfu moja mia nane na thelathini na mbili—

12 Kwa uwezo wa aRoho bmacho yetu yalifunguliwa na ufahamu wetu ukatiwa nuru, nasi tukaona na kuyaelewa mambo ya Mungu—

13 Hata mambo yale yaliyokuwa mwanzo kabla ya ulimwengu kuwako, yaliyowekwa na Baba, kupitia Mwanawe wa Pekee, ambaye alikuwa kifuani mwa Baba, hata kutoka amwanzo;

14 Ambaye sisi tunamshuhudia; na ushuhuda tunaoutoa ni utimilifu wa injili ya Yesu Kristo, ambaye ndiye Mwana, tuliyemwona na ndiye atuliyeongea naye katika bono la mbinguni.

15 Kwani wakati tulipokuwa tukifanya kazi ya akutafsiri, ambayo Bwana alitupangia, tulikuja kwenye mstari wa ishirini na tisa wa mlango wa tano wa Yohana, ambayo ilitolewa kama ifuatavyo—

16 Ukizungumzia juu ya ufufuko wa wafu, kuhusu wale watakao aisikia sauti ya bMwana wa Mtu:

17 Na watatoka; wale waliofanya amema, kwa bufufuo wa wenye chaki; na wale waliotenda uovu, kwa ufufuo wa wasio na haki.

18 Sasa hili lilitufanya sisi tustaajabu, kwa kuwa lilitolewa kwetu na Roho.

19 Na wakati atukitafakari mambo haya, Bwana aligusa macho ya ufahamu wetu nayo yakafunguka, na utukufu wa Bwana ukangʼaa pande zote.

20 Nasi tukauona autukufu wa Mwana, akiwa bmkono wa kuume wa cBaba, na kupokea utimilifu wake;

21 Na tukawaona amalaika watakatifu, na wale bwaliotakaswa mbele ya kiti chake cha enzi, wakimwabudu Mungu, na Mwanakondoo, ambao chumwabudu yeye milele na milele.

22 Na sasa, baada ya ushuhuda mwingi uliokwisha kutolewa juu yake, huu ni aushuhuda, wa mwisho wa zote, ambao tunautoa juu yake: Kwamba byu hai!

23 Kwani atulimwona, hata mkono wa kuume wa bMungu; na tukasikia sauti ikitushuhudia kuwa yeye ndiye cMzaliwa Pekee wa Baba—

24 Kwamba kwa ayeye, na kwa njia yake, na kutoka kwake, bdunia zipo na ziliumbwa, na waliomo ni cwana na mabinti wa Mungu.

25 Na hii tuliona pia, na tunalishuhudia, kwamba amalaika wa Mungu aliye kuwa mwenye mamlaka katika uwepo wa Mungu, ambaye aliasi dhidi ya Mwana Pekee ambaye Baba alimpenda na ambaye alikuwa katika kifua cha Baba, alitupwa chini kutoka katika uwepo wa Mungu na Mwana,

26 Na aliitwa Mpotevu, kwa kuwa mbingu zililia juu yake—alikuwa aLusiferi, mwana wa asubuhi.

27 Nasi tuliona, na lo, aameanguka! ameanguka, hata yule mwana wa asubuhi!

28 Na wakati tukiwa bado katika Roho, Bwana alituamuru kuwa tuliandike ono hili; kwani tulimwona Shetani, yule anyoka wa zamani, aitwaye bibilisi, ambaye calimwasi Mungu, na anataka kuutoa ufalme wa Mungu wetu na Kristo wake—

29 Kwa hiyo, yeye hufanya avita na watakatifu wa Mungu, na kuwazingira.

30 Na tuliona ono la mateso ya wale ambao alifanya vita nao na kuwashinda, kwani hivi ndivyo sauti ya Bwana ilikuja kwetu:

31 Hivyo ndivyo asemavyo Bwana kuhusu wale wote wanaojua uwezo wangu, na kufanywa washiriki wake, na wakaruhusu uwezo wa ibilisi auwashinde, na kuukana ukweli na kuukataa uwezo wangu—

32 Hao ndiyo walio awana wa bupotevu, ambao ndiyo nisemao kuwa ingekuwa heri kwao kama wasingalizaliwa;

33 Kwani wao ni vyombo vya ghadhabu, vilivyohukumiwa kuteseka kwa ghadhabu ya Mungu, pamoja na ibilisi na malaika zake milele;

34 Kuhusu niliyemsema hakuna amsamaha katika ulimwengu huu wala katika ulimwengu ujao—

35 Akiwa aamemkana Roho Mtakatifu baada ya kumpokea, na kumkana Mwana Pekee wa Baba, kwa kuwa bwanamsulubisha kwa nafsi zao na kumfedhehesha kwa dhahiri.

36 Hawa ndiyo wale ambao watakwenda katika aziwa la moto na kiberiti, pamoja na ibilisi na malaika zake—

37 Na hao ndiyo pekee ambao amauti ya pili yatakuwa na uwezo juu yao;

38 Ndiyo, amini, ahao ndiyo pekee ambao hawatakombolewa wakati wa Bwana ufikapo, baada ya kuteseka kwa ghadhabu yake.

39 Kwani wote waliobakia awatarejeshwa kwa bufufuko wa wafu, kwa ushindi na utukufu wa cMwanakondoo, aliyechinjwa, aliyekuwa katika kifua cha Baba kabla ya dunia hazijaumbwa.

40 Na hii ndiyo ainjili, habari njema, ambayo sauti kutoka mbinguni ilitushuhudia—

41 Kwamba alikuja duniani, hata Yesu, ili akusulubiwa kwa ajili ya ulimwengu, na bkuchukua dhambi za culimwengu, na dkuutakasa ulimwengu, na ekuusafisha kutokana na udhalimu wote;

42 Ili kupitia kwake yeye wote wapate akuokolewa wale ambao Baba aliwaweka katika uwezo wake na kuumbwa naye;

43 Yule amtukuzaye Baba, na kuokoa kazi zote za mikono yake, isipokuwa wale wana wa upotevu wanaomkana Mwana baada ya Baba kumfunua.

44 Kwa hiyo, yeye huwaokoa wote isipokuwa wao—watakwenda zao kuingia katika adhabu isiyo na mwisho, ambayo ni aadhabu bbila mwisho, ambayo ni adhabu ya milele, kutawala na cibilisi na malaika wake milele, mahali ambamo dfunza wao hawafi, wala moto hauzimiki, ambayo ndiyo mateso yao—

45 Na amwisho wake, wala mahali pake, wala mateso yao, hakuna mwanadamu ajuaye;

46 Wala haikufunuliwa, wala haifunuliwi, na wala haitafunuliwa kwa mwanadamu, isipokuwa kwao wao washiriki wake;

47 Hata hivyo, Mimi, Bwana, nawaonyesha wengi kwa ono, lakini nafunga tena mara moja;

48 Kwa hiyo, mwisho, upana, urefu, akina na uchungu wake, hawaufahamu, wala hapana mtu yeyote isipokuwa wale bwaliotawazwa kwa chukumu hii.

49 Na tulisikia sauti ikisema: Andikeni ono hili, kwani lo, huu ndiyo mwisho wa ono la mateso ya wasiomcha Mungu.

50 Na tena, tunatoa ushuhuda—kuwa tuliona na kusikia, na huu ni aushuhuda wa injili ya Kristo kuhusu wao watakaotokea katika bufufuko wa wenye haki—

51 Hawa ni wale ambao wameupokea ushuhuda wa Yesu, na akuliamini jina lake, na bwakabatizwa kwa cjinsi ya kuzikwa kwake, kwa dkuzikwa majini katika jina lake, na hii ni sawa na amri ambazo amezitoa—

52 Kwa kushika amri waweze akuoshwa na bkusafishwa kutokana na dhambi zao zote, na kumpokea Roho Mtakatifu kwa kuwekewa cmikono na yule ambaye dametawazwa na kufungwa kwa euwezo huu;

53 Na ambaye hushinda kwa imani, na akutiwa muhuri na bRoho Mtakatifu wa ahadi, ambaye Baba humpeleka juu ya wale wote walio haki na kweli.

54 Hawa ndiyo wale walio wa kanisa la aMzaliwa wa Kwanza.

55 Hawa ndiyo wale ambao Baba amewapa vitu avyote mikononi mwao—

56 Hawa ndiyo wale walio amakuhani na wafalme, ambao wamepokea utimilifu wake, na utukufu wake;

57 Na ni makuhani wa aAliye Juu Sana, kwa mfano wa Melkizedeki, ambaye alikuwa kwa mfano wa bHenoko, ambaye alikuwa kwa cmfano wa Mwana Pekee.

58 Kwa hiyo, kama vile ilivyoandikwa, wao ndiyo amiungu, hata bwana wa cMungu

59 Kwa hiyo, vitu avyote ni mali yao, iwe uzima au mauti, au vile vilivyopo, au vile vitakavyo kuwepo, vyote ni vyao nao ni wa Kristo, na Kristo ni wa Mungu.

60 Nao awatavishinda vitu vyote.

61 Kwa sababu hii, mtu yeyote na aasijisifie mwanadamu, bali na bajisifie katika Mungu, ambaye catawaweka maadui zake wote chini ya miguu yake.

62 Hawa awatakaa katika buwepo wa Mungu na Kristo wake milele na milele.

63 Hawa ndiyo awale watakaokuja pamoja naye, wakati bakija na mawingu ya mbinguni ckutawala dunia na watu wake.

64 Hawa ndiyo wale watakao kuwa na sehemu katika aufufuo wa kwanza.

65 Hawa ndiyo wale watakao toka katika aufufuo wa wenye haki.

66 Hawa ndiyo wale walioufikia aMlima bSayuni, na mji wa Mungu aliye hai, mahali pa mbinguni, patakatifu pa patakatifu.

67 Hawa ndiyo wale ambao wamefikia majeshi ya malaika yasiyo hesabika kwa mkutano mkuu na kanisa la aHenoko, na la bMzaliwa wa Kwanza.

68 Hawa ndiyo wale ambao majina yao ayameandikwa mbinguni, mahali ambako Mungu na Kristo ni bwaamuzi wa wote.

69 Hawa ndiyo wale watu awenye haki bwaliokamilishwa kwa njia ya Yesu aliye mpatanishi wa cagano jipya, aliye kamilisha dupatanisho huu mkamilifu kwa njia ya umwagikaji wa edamu yake yeye mwenyewe.

70 Hawa ndiyo wale ambao miili yao ni ya aselestia, ambayo butukufu wake ni ule wa cjua, hata utukufu wa Mungu, wa juu kuliko wote, utukufu ambao umeandikwa ukifananishwa kama mwangaza wa jua la angani.

71 Na tena, tuliona ulimwengu wa aterestria, na tazama na lo, hawa ndiyo wale ambao ni wa terestria, ambao utukufu wao ni tofauti na wale wa kanisa la Mzaliwa wa Kwanza ambao wameupokea utimilifu wa Baba, hata kama ule wa bmwezi unavyo tofautiana na jua la angani.

72 Tazama, hawa ndiyo wale ambao walikufa apasipo na bsheria;

73 Na pia ndiyo aroho za watu waliowekwa bkifungoni, ambao Mwana aliwatembelea, na ckuwahubiria dinjili, ili kwamba wahukumiwe katika mwili kama wahukumiwavyo wanadamu;

74 Na ni wale ambao hawakuupokea aushuhuda wa Yesu katika mwili, lakini baadaye waliupokea.

75 Hawa ndiyo wale ambao ni watu wenye kuheshimiwa duniani, ambao walipofushwa kwa ujanja wa wanadamu.

76 Hawa ndiyo wale ambao hupata utukufu wake, lakini siyo utimilifu wake.

77 Hawa ndiyo wale ambao hupata uwepo wa Mwana, lakini siyo utimilifu wa Baba.

78 Kwa hiyo, wana amiili ya terestria, na siyo miili ya selestia, na hutofautiana katika utukufu kama vile mwezi unavyo tofautiana na jua.

79 Hawa ndiyo wale ambao si amajasiri katika ushuhuda wa Yesu; kwa hiyo, hawatapokea taji la utukufu wa ufalme wa Mungu wetu.

80 Na sasa huu ndiyo mwisho wa ono ambalo tuliliona la miili ya terestria, ambalo Bwana alituamuru sisi kuandika wakati tulipokuwa bado katika Roho.

81 Na tena, tuliona utukufu wa atelestia, ambao ni utukufu ulio mdogo, kama vile utukufu wa nyota unavyo tofautiana na ule utukufu wa mwezi katika anga.

82 Hawa ndiyo wale ambao hawakuipokea injili ya Kristo, wala aushuhuda wa Yesu.

83 Hawa ndiyo wale ambao hawamkatai Roho Mtakatifu.

84 Hawa ndiyo wale watupwao chini ajehanamu.

85 Hawa ndiyo wale ambao hawatakombolewa kutoka kwa aibilisi hadi bufufuo wa mwisho, hadi Bwana, hata Kristo cMwanakondoo, atakapomaliza kazi yake.

86 Hawa ndiyo wale ambao hawapokei utimilifu wake katika ulimwengu wa milele, ila wa Roho Mtakatifu kwa njia ya huduma ya terestria;

87 Na wa terestria kwa njia ya ahuduma ya selestia.

88 Na pia wa telestia hupata kuhudumiwa na malaika ambao wameteuliwa kwa ajili ya kuwahudumia wao, au wale ambao huteuliwa kuwa roho watumikao kwa ajili yao; kwa kuwa watakuwa warithi wa wokovu.

89 Na hivi tuliona, katika ono la mbinguni, utukufu wa telestia, ipitayo akili zote;

90 Na hakuna mtu ajuaye isipokuwa yule ambaye Mungu amemfunulia.

91 Na hivi tuliona utukufu wa terestria iizidiyo katika kila kitu utukufu wa telestia, hata katika utukufu, na katika uwezo, na katika nguvu, na katika utawala.

92 Na hivi tuliona utukufu wa selestia, ukizidi nyingine katika vitu vyote—mahali ambapo Mungu, hata Baba, hutawala juu ya kiti chake cha enzi milele na milele;

93 Ambaye mbele ya kiti chake cha enzi vitu vyote husujudu kwa upole na aunyenyekevu, na kumpa yeye utukufu milele na milele.

94 Wale waishio katika auwepo wake ni wa kanisa la bMzaliwa wa Kwanza; nao huona kama wanavyoonekana, na ckujua kama wanavyojulikana, wakiwa wamepokea utimilifu wake na dneema yake;

95 Naye huwafanya kuwa asawa katika uwezo, na katika nguvu, na katika utawala.

96 Na utukufu wa selestia ni moja, kama vile utukufu wa ajua ni mbali.

97 Na utukufu wa terestria ni mmoja, kama vile utukufu wa mwezi ni mbali.

98 Na utukufu wa telestia ni mmoja, kama vile utukufu wa nyota ni moja; maana iko tofauti ya utukufu hata kati ya utukufu wa nyota na nyota katika ulimwengu wa telestia.

99 Kwani hawa ndiyo wale ambao ni wa aPaulo, na Apolo, na wa Kefa.

100 Hawa ndiyo wale ambao husema kuna wale wa huyu na wengine wa mwingine—wengine wa Kristo na wengine wa Yohana, na wengine wa Musa, na wengine wa Elia, na wengine wa Esaya, na wengine wa Isaya, na wengine wa Henoko;

101 Lakini hawakuipokea injili, wala ushuhuda wa Yesu, wala manabii, wala aagano lisilo na mwisho.

102 Mwisho wa wote, hawa wote ni wale ambao hawatakusanywa pamoja na watakatifu, akulakiwa kwenye bkanisa la Mzaliwa wa Kwanza, na kupokelewa mawinguni.

103 Hawa ndiyo awale bwaongo, na wachawi, na cwazinzi, na makahaba, na yeyote apendaye na kufanya uwongo.

104 Hawa ndiyo wale ambao huteseka kwa aghadhabu ya Mungu duniani.

105 Hawa ndiyo wale ambao ahuadhibiwa kwa moto wa milele.

106 Hawa ndiyo wale ambao hutupwa chini ajehanamu na bkuteseka na ghadhabu ya cMwenyezi Mungu, hadi wakati dmtimilifu, wakati Kristo a etakapowaweka maadui zake wote chini ya miguu yake, na fkukamilisha kazi yake;

107 Wakati atakapoutoa ufalme, na kuukabidhi kwa Baba, pasipo doa, akisema: Nimeshinda na analikanyaga bkinu peke yangu, hata kinu cha kushindikia mvinyo wa ghadhabu ya Mwenyezi Mungu.

108 Ndipo atakapovikwa taji la utukufu wake, na kukaa juu ya akiti cha enzi ya uwezo wake na kutawala milele na milele.

109 Lakini tazama, na lo, tuliona utukufu na wakazi wa ulimwengu wa telestia, kwamba walikuwa hawahesabiki kama vile nyota katika anga la mbingu, au kama mchanga ulio ufukoni mwa bahari;

110 Na tulisikia sauti ya Bwana ikisema: Hawa wote watapiga magoti, na kila ulimi autakiri kwake aketiye juu ya kiti cha enzi milele na milele;

111 Kwani watahukumiwa kulingana na matendo yao, na kila mtu atapokea kulingana na amatendo yake, na utawala wake, katika bmakao yaliyotayarishwa;

112 Nao watakuwa watumishi wa Aliye Juu Sana; lakini amahali Mungu na Kristo bwakaapo hawawezi kuja, milele na milele.

113 Huu ni mwisho wa ono ambalo tuliliona, ambalo tuliamriwa kuliandika wakati tulipokuwa bado katika Roho.

114 Lakini ni amakuu na ya ajabu matendo ya Bwana, na bsiri za ufalme wake ambazo alizionyesha kwetu, ambazo hupita akili zote katika utukufu, na katika nguvu, na katika utawala;

115 Ambayo alituamuru tusiyaandike wakati tulipokuwa tungali katika Roho, na ambayo ahajaruhusu mwanadamu ayanene;

116 Wala mwanadamu ahawezi kuyafunua, kwani ni ya kuonwa tu na bkueleweka kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, ambaye Mungu huwapa wale wampendao, na kuwatakasa mbele zake;

117 Hao huwapa heshima hii ya kuona na kutambua wenyewe;

118 Ili kwa njia ya uwezo na mafunuo ya Roho, wakati wakiwa katika mwili, waweze kustahili uwepo wake katika ulimwengu wa utukufu.

119 Na utukufu, na heshima, na utawala vina Mungu na Mwanakondoo, milele na milele. Amina.