Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 85


Sehemu ya 85

Ufunuo uliotolewa kupitia Joseph Smith Nabii, huko Kirtland, Ohio, tarehe 27 Novemba 1832. Sehemu hii ni dondoo kutoka barua ya Nabii aliyo mwandikia William W. Phelps, ambaye alikuwa akiishi Independence, Missouri. Ilitolewa ili kujibu maswali juu ya wale Watakatifu waliokwisha hamia Sayuni lakini hawakuwa wamefuata amri ya kuweka wakfu mali zao na hivyo hawakupokea urithi wao kulingana na utaratibu uliowekwa katika Kanisa.

1–5, Urithi katika Sayuni utapokelewa kwa njia ya kuwekwa wakfu; 6–12, Mmoja aliye hodari na mwenye nguvu atawapa Watakatifu urithi wao katika Sayuni.

1 Ni kazi ya karani wa Bwana, aliyemteua, kuhifadhi historia, na akumbukumbu ya jumla ya kanisa ya mambo yote yatendekayo katika Sayuni, na juu ya wale wote ambao huweka mali yao bwakfu, na kupokea urithi kisheria kutoka kwa askofu;

2 Na pia namna wanavyoishi, imani yao na matendo yao; na pia waasi wanaoasi baada ya kupokea urithi wao.

3 Ni kinyume cha mapenzi na amri ya Mungu kwamba wale ambao hawapati urithi wao kwa akuwekwa wakfu, kulingana na sheria yake, ambayo ametoa, ili aweze bkuwalipisha zaka watu wake, ili kuwaandaa wao dhidi ya siku ile ya ckisasi na kuchomwa, wawe na majina yao yakiwa yameorodheshwa pamoja na watu wa Mungu.

4 Wala nasaba yao isiwekwe, au isiwepo mahali ambapo itaweza kupatikana katika kumbukumbu yoyote au historia ya kanisa.

5 Majina yao hayatapatikana, wala majina ya baba zao, wala majina ya watoto hayataandikwa katika akitabu cha sheria ya Mungu, asema Bwana wa Majeshi.

6 Ndiyo, hivyo ndivyo yasemavyo asauti ndogo tulivu, ambayo hunongʼona na bkupenya vitu vyote, na mara nyingi huifanya mifupa yangu itetemeke wakati ijitokezapo, yakisema:

7 Na itakuwa kwamba Mimi, Bwana Mungu, nitamtuma mmoja hodari na mwenye nguvu, akishika fimbo ya mamlaka katika mkono wake, amejivika nuru kama vazi, ambaye kinywa chake kitanena maneno, maneno ya milele; kwa maana matumbo yake yatakuwa chemichemi ya ukweli, ili kuiweka katika utaratibu nyumba ya Mungu, na kupanga kwa kupiga kura urithi wa watakatifu ambao majina yao yanapatikana, na majina ya baba zao, na ya watoto wao, yameorodheshwa katika kitabu cha sheria ya Mungu;

8 Kwa maana mtu yule, aliyeitwa na Mungu na kuteuliwa, kwamba aunyoshe mkono wake ili kulitegemeza asanduku la Mungu, ataanguka kwa mshale wa mauti, kama vile mti uliopigwa kwa mshale wa radi.

9 Na wale wote ambao hawakuandikwa katika akitabu cha kumbukumbu hawatapata urithi katika siku ile, bali watatengwa, na kuwekewa fungu lao miongoni mwa wasioamini, ndiko kutakuwako na bkilio na kusaga meno.

10 Mambo haya siyaneni kwa nafsi yangu tu; kwa hiyo, kama vile Bwana anenavyo, yeye pia atatimiza.

11 Na wale wa Ukuhani Mkuu, ambao majina yao hayapatikani kuwa yameandikwa katika akitabu cha sheria, au ambao wamepatikana kuwa bwamekengeuka, au kuwa cwametengana na kanisa, vile vile wa ukuhani mdogo, au waumini, katika siku ile hawatapata urithi miongoni mwa watakatifu wa Aliye Juu Sana;

12 Kwa hiyo, itafanyika kwao kama vile kwa watoto wa kuhani, kama itakavyoonekana kuandikwa katika mlango wa pili na mstari wa sitini na moja na sitini na mbili wa Ezra.