Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 80


Sehemu ya 80

Ufunuo uliotolewa kupitia Joseph Smith Nabii, kwenda kwa Stephen Burnett, Hiram, Ohio, Machi 7, 1832.

1–5, Stephen Burnett na Eden Smith wanaitwa kuhubiri katika mahali popote watakapochagua.

1 Amini, hivyo ndivyo asemavyo Bwana kwako wewe mtumishi wangu Stephen Burnett: Nenda wewe, nenda wewe ulimwenguni na ukahubiri injili kwa kila kiumbe kitakachokuwa chini ya sauti yako.

2 Na kwa vile unataka mwenza, nitakupa mtumishi wangu Eden Smith.

3 Kwa hiyo, nendeni na mkaihubiri injili yangu, iwe kaskazini au kusini, mashariki au magharibi, si kitu, kwani hamwezi kukosea.

4 Kwa sababu hiyo, yatangazeni mambo ambayo mmeyasikia, na hakika kuyaamini, na kujua ni ya kweli.

5 Tazama, haya ndiyo mapenzi yake yeye aliyewaita ninyi, Mkombozi wenu, hata Yesu Kristo. Amina.