Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 83


Sehemu ya 83

Ufunuo uliotolewa kupitia kwa Joseph Smith Nabii, huko Independence, Missouri, 30 Aprili 1832. Ufunuo huu ulipokelewa wakati Nabii alipokuwa amekaa katika baraza pamoja na viongozi wenzake wa kanisa.

1–4, Wanawake na watoto wanayo haki ya kudai matunzo kutoka kwa waume na baba zao; 5–6, Wajane na yatima wanayo haki ya kupata matunzo kutoka katika Kanisa.

1 Amini, hivyo ndivyo asemavyo Bwana, kwa nyongeza kwenye sheria za kanisa kuhusu wanawake na watoto, wale ambao ni wa kanisa, ambao awamewapoteza waume au baba zao:

2 Wanawake wanayo ahaki ya matunzo kutoka kwa waume wao, hadi waume wao watapochukuliwa; na kama hawakupatikana kuwa wavunjaji wa sheria watapata ushirika katika kanisa.

3 Na kama siyo waaminifu hawatapata ushirika katika kanisa; ingawa wanaweza kubaki juu ya urithi wao kulingana na sheria za nchi.

4 aWatoto wote wanayo haki juu ya wazazi wao kwa ajili ya matunzo hadi wafikiapo umri wa kujitegemea.

5 Na baada ya hapo, wanakuwa na haki juu ya kanisa, au katika maneno mengine juu ya aghala ya Bwana, ikiwa wazazi wao hawana chochote cha kuwapa kuwa urithi wao.

6 Na ghala itatunzwa kwa mali iliyowekwa wakfu na kanisa; na awajane na yatima watatunzwa kwa mali hiyo, kama pia bmaskini. Amina.