Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 73


Sehemu ya 73

Ufunuo uliotolewa kwa Joseph Smith Nabii na Sidney Rigdon, huko Hiram, Ohio, tarehe 10 10 Januari 1832. Kutoka mwanzoni mwa Desemba iliyotangulia, Nabii na Sidney walikuwa wamejishughulisha katika kuhubiri, na kwa njia hii inamaanisha walikamilisha mengi katika kupunguza hisia zisizo nzuri ambazo zilijitokeza dhidi ya Kanisa (ona kichwa cha habari cha sehemu ya 71).

1–2, Wazee waendelee kuhubiri; 3–6, Joseph Smith na Sidney Rigdon wataendelea kutafsiri Biblia hadi imalizike.

1 Kwani amini, hivyo ndivyo asemavyo Bwana, yafaa kwangu kwamba awaendelee kuhubiri injili, na katika kuyashawishi makanisa katika maeneo ya jirani, hadi wakati wa mkutano;

2 Na halafu, tazama, itajulikana kwao, kwa asauti ya mkutano, juu ya kazi zao mbalimbali.

3 Sasa, amini ninawaambia watumishi wangu, Joseph Smith, Mdogo, na Sidney Rigdon, asema Bwana, ni amuhimu kwenu bkutafsiri tena;

4 Na, ilimradi yawezekana, kuhubiri katika maeneo ya jirani hadi mkutano ujao; na baada ya hapo ni muhimu ninyi kuendelea na kazi ya kutafsiri hadi imalizike.

5 Na huu uwe ni utaratibu kwa wazee hadi itakapojulishwa vinginevyo, hata kama ilivyoandikwa.

6 Sasa sitatoa zaidi kwenu kwa wakati huu. aVifungeni viuno vyenu na kuwa na kiasi. Hivyo ndivyo. Amina.