Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 17


Sehemu ya 17

Ufunuo uliotolewa kupitia Joseph Smith Nabii kwa Oliver Cowdery, David Whitmer, na Martin Harris, huko Fayette, New York, Juni 1829, kabla ya kuona mabamba ya michoro ambayo yalikuwa na kumbukumbu ya Kitabu cha Mormoni, Joseph na mwandishi wake, Oliver Cowdery, walijifunza kutoka kwenye tafsiri ya Kitabu cha Mormoni kwamba mashahidi watatu maalumu watateuliwa (ona Etheri 5:2–4; 2 Nefi 11:3; 27:12). Oliver Cowdery, David Whitmer, na Martin Harris waliongozwa kwa kushawishika kutaka kuwa mashahidi watatu maalumu. Nabii alimwuliza Bwana, na ufunuo huu ulitolewa kama jibu kupitia Urimu na Thumimu.

1–4, Kwa imani Mashahidi Watatu hao watayaona mabamba na vitu vingine vitakatifu; 5–9, Kristo atoa ushuhuda wa utakatifu wa Kitabu cha Mormoni.

1 Tazama, ninawaambia, kwamba ni lazima ninyi mtegemee maneno yangu, ambayo kama mtafanya kwa dhamira ya moyoni, mtapata kuona mabamba hayo, na pia dera ya kifua, upanga wa Labani, Urimu na Thumimu, ambavyo vilitolewa kwa kaka wa Yaredi juu ya mlima, wakati alipozungumza na Bwana uso kwa uso, na vielekezi vya kimiujiza ambavyo alipewa Lehi akiwa nyikani, mpakani mwa Bahari ya Shamu.

2 Na ni kwa imani yenu kwamba mtapata kuyaona hayo, hata kwa imani ile ambayo ilikuwa kwa manabii wa kale.

3 Na baada ya hapo mmekwishapata imani, na mmeyaona hayo kwa macho yenu, mtayashuhudia hayo, kwa nguvu za Mungu.

4 Na hii ninyi mtafanya ili kwamba mtumishi wangu Joseph Smith, Mdogo, asiangamizwe, kwamba niweze kutimiza madhumuni yangu ya haki kwa wanadamu katika kazi hii.

5 Na mtashuhudia kwamba mmeyaona, hata vile mtumishi wangu Joseph Smith, Mdogo, alivyoyaona; kwani ni kwa uwezo wangu kwamba ameyaona, na ni kwa sababu alikuwa na imani.

6 Na amekwisha tafsiri kitabu, hata sehemu ile ambayo nilimwamuru, na kama vile Bwana wenu na Mungu wenu aishivyo ni kweli.

7 Kwa hiyo, ninyi mmepokea uwezo ule ule, na imani ile ile, na kipawa kile kile kama yeye;

8 Na kama mtafanya amri zangu hizi za mwisho, ambazo nimewapa ninyi, milango ya jehanamu haitawashinda; kwani neema yangu inawatosha, na ninyi mtainuliwa siku ya mwisho.

9 Na Mimi, Yesu Kristo, Bwana wenu na Mungu wenu, nimesema hayo kwenu ninyi, ili kwamba niweze kutimiza madhumuni yangu ya haki kwa wanadamu. Amina.

Chapisha