Ono lililotolewa kwa Joseph Smith Nabii na Sidney Rigdon, huko Hiram, Ohio, 16 Februari 1832. Katika utangulizi wa kumbukumbu ya ono hili, Historia ya Joseph Smith inaeleza: “Baada ya kurejea kutoka kwenye mkutano huko Amherst, nilianza tena tafsiri ya Maandiko. Kutokana na mafunuo mbali mbali ambayo nilikuwa nimekwisha yapokea, ilionekana dhahiri kwamba vipengele vingi muhimu vinavyogusa wokovu wa mwanadamu, vilikuwa vimeondolewa kutoka kwenye Biblia, au vilipotezwa kabla haijatungwa. Ilionekana wazi kutokana na ukweli uliosalia, kwamba kama Mungu alimzawadia kila mtu kulingana na matendo aliyoyafanya katika mwili neno ‘Mbingu,’ kama linavyo kusudiwa na Watakatifu kuwa makao ya milele, ni lazima ziwe falme zaidi ya moja. Vivyo hivyo, … wakati nikitafsiri injili ya Mt. Yohana, mimi mwenyewe na Mzee Rigdon tuliona ono lifuatalo” Wakati ono hili likitolewa, Nabii alikuwa akitafsiri Yohana 5:29.