Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 99


Sehemu ya 99

Ufunuo uliotolewa kupitia Joseph Smith Nabii kwa John Murdock, 29 Agosti 1832, huko Hiram, Ohio. Kwa zaidi ya mwaka mmoja, John Murdock amekuwa akihubiri injili wakati watoto wake—wasio na mama baada ya kifo cha mke wake, Julia Clapp, Aprili 1831—wakikaa na familia nyingine huko Ohio.

1–8, John Murdock anaitwa kutangaza injili, na wale wanaompokea, wanampokea Bwana na watapata rehema.

1 Tazama, hivyo ndivyo asemavyo Bwana kwa mtumishi wangu John Murdock—wewe umeitwa kwenda katika nchi za mashariki kutoka nyumba hadi nyumba, kutoka kijiji hadi kijiji, na kutoka mji hadi mji, kutangaza injili yangu isiyo na mwisho kwa wakazi wake, katikati ya amateso na uovu.

2 Na yule aakupokeaye wewe anipokea Mimi; nawe utapata nguvu za kulitangaza neno langu kwa bdalili za Roho wangu Mtakatifu.

3 Na yule akupokeaye wewe akama mtoto mdogo, huupokea bufalme wangu; na heri yao, kwa maana watapata crehema.

4 Na yeyote akukataaye wewe aatakataliwa na Baba yangu na nyumba yake; nawe utayakungʼuta mavumbi ya bmiguu yako katika mahali pa siri kando ya njia kwa ushuhuda dhidi yao.

5 Na tazama, na lo, anaja haraka kwa bhukumu, na kuwadhibitishia wote matendo yasiyo ya ucha Mungu juu ya matendo ambayo wametenda dhidi yangu, kama ilivyoandikwa katika gombo la chuo.

6 Na sasa, amini ninakuambia, kuwa haifai kwamba uende sasa hadi watoto wako wapate mahitaji yao, na kuwapeleka kwa askofu wa Sayuni.

7 Na baada ya miaka michache, kama utanitamani, utaweza pia kwenda katika nchi iliyo nzuri, ili kumiliki urithi wako;

8 Vinginevyo wewe utaendelea kutangaza injili yangu ahadi utakapochukuliwa. Amina.