Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 134


Sehemu ya 134

Tamko la imani kuhusu serikali na sheria kwa ujumla, lililokubaliwa kwa kura nyingi kwenye mkutano mkuu wa Kanisa uliofanyika huko Kirtland, Ohio, 17 Agosti 1835. Watakatifu wengi walikusanyika pamoja kutafakari mapendekezo ya maudhui ya toleo la kwanza la Mafundisho na Maagano. Kwa wakati huo, tamko hilo lilipewa dibaji ifuatayo: “Ili imani yetu juu ya serikali za kidunia na sheria kwa ujumla zisipate kutafsiriwa vibaya au kueleweka vibaya, tumefikiri ni vyema kutoa, mwishoni mwa kitabu hiki, maoni yetu kuhusiana na jambo hilo.”

1–4, Serikali zinapaswa kulinda uhuru wa mawazo na wa kuabudu; 5–8, Watu wote wanapaswa kuziunga mkono serikali zao na kutoa heshima na staha kwa sheria zake; 9–10, Jumuiya za kidini hazipaswi kuwa na mamlaka ya kiserikali; 11–12, Wanadamu wanahalalishwa katika kujitetea wenyewe na mali zao.

1 Sisi tunaamini kwamba aserikali zimewekwa na Mungu kwa manufaa ya mwanadamu; na kwamba banawawajibisha wanadamu kwa matendo yao kuhusiana nazo, katika kutunga sheria na kuzitekeleza, kwa faida na usalama wa jamii.

2 Sisi tunaamini kwamba hakuna serikali inayoweza kudumu katika amani, isipokuwa sheria hizo zimetungwa na kutunzwa bila kuvunjwa ambazo zitamhakikishia kila mtu auhuru wa bmawazo, haki na udhibiti wa mali yake, na culinzi wa maisha yake.

3 Sisi tunaamini kwamba serikali zote zinahitaji kuwa na amaofisa wake, na mahakimu ili kuzitekeleza sheria hizo; na ni aina ya maofisa ambao wataitekeleza sheria katika usawa na haki yapaswa watafutwe na kuungwa mkono kwa sauti ya watu kama ni jamhuri, au kwa ridhaa ya wenye nchi.

4 Sisi tunaamini kwamba dini imewekwa na Mungu; na kwamba wanadamu wanawajibika kwake, na ni kwake pekee yake, kwa kuitekeleza, isipokuwa kama dhana za dini yao zinachochea juu ya kuvunja haki na uhuru wa wengine; lakini hatuamini kwamba sheria za kibinadamu zinayo haki ya kuingilia katika kutoa taratibu za jinsi ya akuabudu ili kufunga uhuru wa mawazo ya wanadamu, wala kuweka taratibu kwa ajili ya watu kuabudu hadharani au sirini; kwamba mahakimu wa serikali wanapaswa kuzuia uvunjaji wa sheria, lakini kamwe hawapaswi kuthibiti uhuru wa mawazo; wanapaswa kuwaadhibu wahalifu, lakini kamwe wasikandamize uhuru wa roho.

5 Sisi tunaamini kwamba wanadamu wote wanalazimika kukubali na kuunga mkono serikali zilizopo ambamo ndani yake wanaishi, wakiwa wanalindwa pamoja na haki zao za msingi haki zisizoondoshwa kwa sheria za serikali hizo, na kwamba uchochezi na auasi si sahihi kwa kila raia ambaye kwa njia hiyo hulindwa, na anapaswa kuadhibiwa sawia; na kwamba serikali zote zinayo haki ya kuzitumia sheria hizo kama ionavyo katika maamuzi yake yenyewe kuwa ni vyema ili kulinda maslahi ya umma; na wakati huo huo, katika hali yoyote, ikishika kitakatifu uhuru wa mawazo.

6 Sisi tunaamini kwamba kila mwanadamu anapaswa kuheshimika katika nafasi yake, kama vile watawala na mahakimu, wakiwa wamewekwa kwa ajili ya ulinzi wa wasio na hatia na kuwaadhibu walio na hatia; na kwamba kwa asheria wanadamu wote wanapaswa kuwapa heshima na staha, kwa vile pasipo wao amani na mapatano vingetawaliwa na vurugu na vitisho; sheria za kibinadamu ziliwekwa hususani kwa madhumuni ya kutawala maslahi yetu kama mtu binafsi na kama taifa, kati ya mtu na mtu; na sheria takatifu zilizotolewa kutoka mbinguni, zikielezea juu ya masuala ya kiroho, kwa ajili ya imani na kuabudu, yote kujibiwa na mwanadamu kwa Muumba wake.

7 Sisi tunaamini kwamba watawala, majimbo, na serikali wanayo haki, na wanalazimika kutekeleza sheria kwa ajili ya kuwalinda wananchi wote katika uhuru wa kutekeleza imani yao ya kidini; lakini hatuamini kwamba wanayo haki kisheria ya kuwanyima wananchi haki yao hii, au kuwakataza wao katika imani yao, ilimradi staha na heshima zinaonyeshwa kwa sheria na imani hiyo ya kidini haitetei uchochezi wala kula njama dhidi ya serikali.

8 Sisi tunaamini kwamba kutendwa kwa uhalifu kunapaswa akuadhibiwa kulingana na aina ya kosa; kwamba mauaji, uhaini, wizi wa kutumia nguvu, wizi, na uvunjaji wa amani kwa ujumla, katika njia yoyote ile, kunapaswa kuadhibiwa kulingana na uzito wa uhalifu wao na mwelekeo wao kwenye uovu miongoni mwa wanadamu, kwa sheria za serikali ile ambamo kosa lile limetendeka; na kwa ajili ya amani na utulivu wa umma watu wote wanapaswa kujitoa na kutumia uwezo wao katika kuwaleta wahalifu mbele ya sheria zilizo nzuri ili kuadhibiwa.

9 Sisi hatuamini kuwa ni haki kuchanganya mvuto wa kidini pamoja na serikali ya kiraia, ambapo jumuiya moja ya kidini itakimiwa na nyingine itakataliwa katika haki zake za kiroho, na haki binafsi za waumini wake, kama wananchi, watanyimwa.

10 Tunaaamini kwamba jumuiya zote za kidini zinayo haki ya kuwashughulikia waumini wake kwa tabia zisizokubalika, kulingana na kanuni na taratibu hizo; ili mradi kushughulika huko ni kwa ajili ya ushirikiano na nia njema; lakini sisi hatuamini kwamba jumuiya yoyote ya kidini inayo mamlaka ya kuwahukumu watu juu ya haki ya mali zao, au uhai wao, kwa kuchukua mali zao za ulimwengu huu, au kuwahatarishia uhai au kiungo, au kutoa adhabu yoyote ya kimwili juu yao. Wanaweza tu akuwatenga kutoka kwenye jumuiya zao, na kuondoa ushirikiano wao.

11 Tunaamini kwamba wanadamu wanapaswa kukata rufaa kwa sheria za nchi kwa ajili ya kufidiwa mabaya na maovu yote, ikiwa mabaya yametendeka kwa mtu au haki ya kumiliki mali au sifa njema imevunjwa, katika mahali ambapo sheria hizi zipo na zitamlinda katika mambo haya; lakini tunaamini kwamba wanadamu wote wanahesabiwa haki katika kujilinda wao wenyewe, marafiki zao, mali, na serikali yao, kutokana na uvamizi usio wa haki na maingiliano ya watu wote nyakati za dharura, wakati ambapo rufaa ya haraka haiwezi kufanyika kwa vyombo vya sheria, na msaada kupatikana.

12 Sisi tunaamini kuwa ni haki akuhubiri injili kwa mataifa yote ya duniani, na kuwaonya wenye haki kujiokoa wenyewe kutokana na uharibifu wa ulimwengu; lakini hatuamini kuwa ni haki kuwaingilia watumwa, wala kuwahubiria injili, wala kuwabatiza kinyume na matakwa na mapenzi ya mabwana wao, wala kuingilia mambo yao au kuwashawishi hata katika kiwango kidogo kuwasababisha wasiridhike na hali yao katika maisha haya, na hivyo kuhatarisha maisha ya watu; kuingilia huko tunaamini kuwa siyo kisheria na siyo haki, na ni hatari kwa amani ya kila serikali inayoruhusu wanadamu kushikiliwa katika utumwa.